Katibu wa itikadi,siasa na uenezi wa CCM taifa Ndugu Humfrey Polepole akitoa semina kwa makatibu wa idara ya Itikadi na uenezi wa mkoa wa Iringa iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo

Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa (MNEC) Salim Asas akiwahutubia makatibu wa idara ya Itikadi na uenezi wa mkoa wa Iringa walikuwa wakipewa semina na Katibu wa itikadi,siasa na uenezi wa CCM taifa Ndugu Humfrey Polepole juu ya Idara hiyo,semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
 Baadhi ya makatibu wa Idara ya Itikadi,siasa na uenezi mkoa wa Iringa wakiwa makini kumsikiza Katibu wa itikadi,siasa na uenezi wa CCM taifa Ndugu Humfrey Polepole alipokuwa anawafunda.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.


Katibu wa itikadi,siasa na uenezi wa CCM taifa Ndugu Humfrey Polepole Amewataka viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia chama hicho kutokuwa chanzo cha migogoro na majungu bali wawe suluhisho kwa kuwa lengo la chama ni kusimamia serikali na kuwaletea watanzania Maendeleo.



ameyasema hayo kwenye semina ya kuwafunda katibu wa Idtikadi na uenzi wa ngazi zote mkoani Iringa, Polepole amesema kuwa kuna baadhi ya viongozi wamekuwa chanzo cha migogoro hata kufanya kurudisha nyuma maendeleo ya chama.



Amesema kuwa chama hicho kimejengwa kwenye misingi bora kwa lengo la kutumikia wananchi na kusikiliza watu pamoja na kujua shida zao lakini kuna baadhi yao wanaleta majungu wao kwa wao jambo linalofanya kutowavumilia.



“Sasa hivi hii ni ccm mpya chini ya mwenyekiti Dr John Pombe Magufuli na hana utani anataka kazi tu na wale ambao wanaona wameshindwa watupishe maana unapoacha sumu ndani si ya siku itakudhuru tunapogombana wanaoumia ni watanzania waliotupa dhamana ya kusimamia serikali”Alisema Polepole



Polepole ameongeza kuwa kwasasa mlango uko wazi endapo mtu anaona atashindwa kupelekana na kasi ya CCM mpya chini ya mwenyekiti wao John Pombe Magufuli ni vyema akapisha na kuacha wanaojua kufanya kazi.

 

Hata hivyo Polepole amewataka viongozi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa huku akimtaka katibu wa itikadi na uenezi mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza kuunganishi vizuri na kuendelea kuwatumikia wananchi vizuri kwa kueleza mambo mazuri yanayofanywa na serikalia ya CCM.



Vile vile Polepole amewasifu viongozi katika ngazi zote kwasababu wameibadilisha ccm na wananchi wameelewa dhamira ya Chama katika kuisimamia serikali.



Aidha Polepole alisema kuwa chama cha mapinduzi kikifanya vibaya kwa wananchi ujue kuwa idara ya Itikadi na uenezi haijafanya kazi yake ipasavyo,hivyo ni lazima kila kiongozi awajibike ipasavyo ili kutimiza malengo ya chama.



“Tunatakiwa kushughulikia matatizo ya wananchi kwa kuwapa mafunzo mbalimbali viongozi wa ngazi za chini ili kueneza vilivyo cha hicho ambacho kipo madarakani muda mrefu sasa” alisema Polepole



Polepole aliwaambia viongozi hao kuwa uongozi ni kujitolea na sio kutegemea kupata maslai furani kwenye chama wakati unagombea nafasi mbalimbali lazima uwe unasehemu ya kuingiza kipato kingine na usitegemee kuvuna kutoka kwenye chama.



Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa (MNEC) Salim Asas alimtaka katibu wa itikadi na uenezi mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza kuratibu namna nyingine tena ya kuwawezesha makatibu hao kuanzia ngazi ya chini hadi juu kupata fedha za kufanyia kazi mafunzo walipata kutoka kwa katibu wa itikadi na uenezi wa CCM taifa Ndugu Humfrey Polepole.



“Ramadhani Baraza nakuomba uratibu zoezi hilo ili tuone jinsi ya kuwasaidia makatibu hao ili waweze kukieneza vilivyo cha chetu kwa wananchi wote huko waliko” alisema Asas



Naye katibu wa itikadi na uenezi mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza alisema ameyapokea maagizo yote na atayafanyia kazi ili idara hiyo mkoa wa Iringa iwe mfano kwa mikoa mingine hapa nchini.
Share To:

Post A Comment: