Sunday, 23 June 2019

ODDO UMMY CUP KURINDIMA LEO KWENYE VIWANJA VYA LAMORE JIJINI TANGA


 Kamishna wa Kinga na Tiba wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Dkt Peter Mfisi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mechi za Kombe la Oddo Ummy Cup zitakazoanza  leo asubuhi June 23 mpaka June 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Lamore Jijini Tanga kulia ni Katibu wa Chama cha Soka mkoa wa Tanga (TRFA) Beatrce Mgaya kushoto ni Mwenyekiti wa Binti Filamu Ndumbaghe Msaya alimaarufu Thea
 Katibu wa Binti Filamu Foundation Joan Matuvolwa kulia akizungumza kushoto ni Katibu wa TRFA Beatrice Mgaya
 Katibu wa Chama cha Mpiwa wa Miguu Mkoa wa Tanga (TRFA) Beatrice Mgaya akizungumza kushoto ni Kamishna wa Kinga na Tiba wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Dkt Peter Mfisi kulia ni  Katibu wa Binti Filamu Foundation Joan Matuvolwa
 Mwenyekiti wa Binti Filamu Ndumbaghe Msaya alimaarufu Thea akizungumza kulia ni Kamishna wa Kinga na Tiba wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Dkt Peter Mfisi
 Kamishna wa Kinga na Tiba wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Dkt Peter Mfisi katikati akikabidhi jezi kwa timu shiriki kwenye mashindano hayo
Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakichukua matukio

MASHINDANO ya Mpira wa Miguu Maalumu kwa ajili ya kuelekea siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Kupambana na Dawa za kulevya nchini Oddo Ummy Cup yanaanza leo kwenye uwanja wa Lamore Jijini Tanga

Mashindano hayo yameandaliwa na Binti Filamu na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye amehakikisha mashindano hayo yanafanyika amekuwa mstari wa mbele kupiga vita dawa za kulevya kuhakikisha vijana hawatumii dawa hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamishna wa Kinga na Tiba wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Dkt Peter Mfisi alisema na mechi zitaanza leo asubuhi June 23 mpaka June 25 mwaka huu.

Alisema kwamba mashindano hayo yatashirikisha timu tano za tatu za wanawaume na mbili za wanawake ambazo zitacheza hatua ya fainali ya mashindano hayo na baadae zitatolewa zawadi na washindi mbalimbali siku ya kilele hicho.

“Kwa kweli nipende kutoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Tanga kujitokeza kwa wingi wapate elimu ambayo itakuwa chachu kwao kuweza kupelekea mabadiliko makubwa kwao “Alisema

Awali akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari Katibu wa Binti Filamu Foundation Joan Matuvolwa alisema binti filamu ni taasisi inayojihusisha wasanii wa kike lengo kufanya shughuli za kijamii kuelekea maadhimisho dawa za kulevya wao waliona waje Tanga kutokana na kwamba Tanga kuwepo kwa takwimu kubwa za watumiaji dawa za kulevya wakaona wafike kutoa elimu.

Alisema wamegundua wameona mpira wa miguu unaweza kuwashirikisha watu wengi hivyo wakashirikiana na Waziri Ummy ndio maana wakaona mashindano hayo yapewe jina hilo wanashirikiana na mamlaka husika.

Hata hivyo aliwakaribisha wakazi wa mkoa wa Tanga kufika kwenye viwanja hivyo kujionea mechi mbalimbali na mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Waziri Ummy.

Naye kwa upande wake Katibu wa Soko Mkoa wa Tanga (TRFA) amesema amefurahishwa na hutua ya Waziri Ummy kwa kuthamini timu husika ambapo zimekabidhiwa vifaa kabla ya michezo hiyo

Katibu huyo alisema michezo hiyo imeshirkisha timu nane ambazo zimegawangwa kwenye makundi mawili yatachezwa kwa mtindo wa mtoano ili kuweza kumpata bingwa.

mwisho

No comments:

Post a Comment