Leo ni siku ya bajeti kwa nchi za Afrika Mashariki, ambapo mawaziri wa fedha wa Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda watawasilisha bajeti za serikali za nchi zao kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Serikali ya Tanzania inapanga kutumia takriban shilingi trilioni 33.1, (dola bilioni 14.3) katika mwaka wa fedha 2019/2020 ikiwa ni ongezeko, kutoka shilingi trilioni 32.5 za Kitanzania katika mwaka wa fedha 2017/2018.

Bajeti ya Kenya, inakadiriwa kuwa dola bilioni 30.2, ambayo ni kubwa kuliko bajeti zote za nchi zingine za afrika mashariki kwa pamoja. Uganda kwa upande wake inakadiria bajeti ya dola bilioni 10.9 huku Rwanda dola bilioni 3.17.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: