Tuesday, 4 June 2019

MWALIMU WA SHULE YA MSINGI AKAMATWA NA SIRAHA YA KIVITA AKIHUSIKA KATIKA UJANGILI.Na Lucas Myovela-Arusha

Jeshi la polisi Mkoani Arusha linamshikilia walimu wa shule ya Msingi ya Naan Bw Solomon Letato (30) mkazi wa Kijiji cha Enguserosambu ,Loliondo wilaya ya Ngorongoro, kwa kuhusika na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha baada ya kukutwa na silaha ya kivita aina ya AK 47 ikiwa na risasi 5.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Mkoani wa Arusha, Jonathan Shanna

Mhuhumiwa huyo akiwa Mtumishi  wa umma alikamatwa Juni 2 mwaka huu,katika kata ya Enguserosambu wilayani Ngorongoro kwa kujihusisha na biashara haramu ya kuingiza silaha za moto kutoka nchi jirani kinyume cha sheria.


Pia kamanda aliezeka kuwa mtuhumiwa huyo ni miongoni mwa wafanya biashara haramu ya nyara za serikali hasa  meno ya tembo pamoja na pembe za Faru .


Wakati huo huo katika.Kijiji cha Mbukeni ,kata ya Arash ,Loliondo Jeshi la Polisi lilifanikiwa kukamata silaha ya kivita  aina ya AK 47 iliyokuwa imetelekezwa katika Kijiji cha Embukeni kufuatia msako mkali wa jeshi la Polisi unaoendelea wilayani humo.


Polisi  inaendelea kuwas√†ka watuhumiwa wanaojihusisha na matukio ya ujambazi na kuwataka wajisalimishe wenyewe  Mara moja kabla hawajafikiwa na mkono wa Polisi.


Katika tukio la jingine kamanda Shana alisema kuwa jeshi hilo limefanikiwa kukamata watuhumiwa watatu wanaojihusisha na uporaji kwa kutumia pikipiki ,ambapo jeshi hilo limefanikiwa kukamata pikipiki nne.


Pikipiki hizo ni pamoja na Namba MC 978CAH aina ya Haojue,MC 559 BHC aina ya Toyo ,MC 427 BKP aina ya Boxer na MC 789 BMC aina ya Boxer na kuwataka wananchi walioibiwa pikipiki wafike kituo cha Polisi kwa ajili ya kuzitambua.


Kamanda aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hamis Juma(37) mkazi wa Ole Matejoo,Isihack Islam (22) mkazi wa Majengo Mkoani Kilimanjaro na Hasan Mushi (54) mkazi wa majengo ,Moshi.


Wakati huo huo jeshi hilo mkoani hapa limempandishwa  kizimbani Jumanne Ally Mjusi baada ya kukamilika kwa upelelezi .


Mjusi alikamatwa Mei 16 mwaka huu akituhumiwa kuvunja na kuiba vitu mbalimbali ikiwemo Bastola aina ya Browng yenye risasi 9 Mali ya Msafiri Msuya .

No comments:

Post a Comment