Mkurugenzi wa Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Rose Reuben ametwaa tuzo ya Wanawake katika Uongozi iliyotolewa na World Women Leaders Congress (WWLC), jijini Dar es Salaam.

Tuzo hiyo ilitolewa 19 kwa wanawake viongozi wa Afrika Mashariki walioleta mabadiliko katika jamii, walioibua vipaji, wanawake mifano ya kuigwa na wenye uthubutu kutoka taasisi na mashirika binafsi na serikali.

Mbali na Rose, mwanamke mwingine aliyetunukiwa tuzo hizo kutoka Tanzania ni Emma Kawawa ambaye Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa Tanzania Women CEO Roundtable. Wanawake viongozi kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi walitunukiwa tuzo hizo kutokana na vigezo vya ushindi vilivyowekwa.

Akizungumzia tuzo hiyo, Rose amesema hatua hiyo inawatia moyo wanawake wengine kufanya bidii.

Wanawake wanaweza kuwa viongozi wazuri, tuzo hii inaeleza kuwa uongozi wa wanawake unakubalika, hii ni tuzo ya dunia, kumbe ulimwengu umekubali kuwa wanawake wanaweza kuwa viongozi,"amesema.

Ameongeza,Jamii kwa ujumla ikubali kuwa wanawake wanaweza kuwa viongozi. Wanahabari wafanye kazi zao kwa kujiamini, kazi zao zikajulikana na wasikatisshwe tamaa na kitu chochote.

Tuzo hizo zinatolewa ili kuhamasisha wanawake viongozi katika sekta za umma na binafsi, kutambua mafanikio ya wanawake kikanda na kidunia pamoja na kuwatia moyo wanawake vijana kushika nafasi za mbalimbali za uongozi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: