Monday, 24 June 2019

MAZOEZI YA MISS TANGA 2019 USIPIME WAKAZI WA MKOA WA TANGA WAMIMINIKA NYUMBANI HOTEL KUWASHUHUDIA

 WAREMBO wanaoshiriki Shindano ya Miss Tanga 2019 wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya mazoezi yao yanayofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Nyumbani leo
 WAREMBO wanaoshiriki Shindano ya Miss Tanga 2019 wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya mazoezi yao yanayofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Nyumbani leo waliokaa mbele katikati ni Muandaaji wa Mashindano hayo Chuchu Hans

NA MWANDISHI WETU, TANGA.

MAZOEZI ya Shindano la Miss Tanga 2019 yameendelea kupamba moto kwenye ukumbi wa Nyumbani Hotel ya Jijini Tanga huku wakazi wa mji huo wakijitokeza kwa wingi kushuhudia kutokana na kusheheni warembo bomba.

Shindano hilo linatarajiwa kufanyika Julai 6 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort iliyopo pembezoni mwa ufukwe wa bahari ya Hindi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Muandaaji wa Shindano hilo Chuchu Hans ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya chuchu Double Touch Entertainment alisema kwamba maandalizi ya shindano.

Alisema kwamba warembo hao wanafanya mazoezi hayo kila siku jioni chini ya Mwalimu wao Pili na Rashida Wanjara

Alisema kwamba katika shindano hilo warembo 18 watachuana ili kuweza kumpata Malkia wa Taji hilo ambayo atauwakilisha mkoa huo kwenye mashindano Kanda ya kaskazini,Miss Tanzania na Shindano la Miss World.

“Kwa kweli kwa sasa maandalizi yanaendelea vizuri na namshukuru Mungu tumepata warembo bomba ambao watashindana kwa lengo la kumpata mshindi wa Kinyang’anyiro hicho “Alisema.

Alisema kabla ya kufanyika kwa shindano hilo warembo hao watashiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kufanya usafi kwenye vituo mbalimbali na vivutio vya Utalii vilivypo mkoani hapa kwa lengo la kuhamasisha utalii wa ndani.

Hata hivyo alisema kwamba onyesho hilo litapambwa na wasanii wa bongo movie na wengine ambao watatumbulishwa na Waandaaji wa Shindano hilo.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment