Tuesday, 4 June 2019

MANOTA ATEMBELEA ZAIDI YA MISKITI 10 KIMARA, AWATAKA WAUMINI KUMSAPOTI JPMDar es Salaam

Diwani wa Kata ya Kimara iliyopo Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam Comredi Paschal Manota kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM amekutana na waumini wa dini ya kiislam pamoja na kutembelea baadhi ya miskiti iliyopo katika kata hiyo

Akizungumza na waumini katika baadhi ya misiki hiyo amewata wananchi wa kimara kuendelea Kuunga mkono juudi za Mhe Rahisi Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kuendeleza upendo baina yetu pasipo kubaguana kwa misingi ya dini na tuendelee kuchapa kazi.

Amesema ameona atembelee misikiti kwa lengo la kuwasalimu lakini pia kuona changamoto zilizoko za kimiundo mbinu na zinginezo kwa kuwa misikiti hiyo iko katika eneo lake la kiutawala kwa hiyo hana budi muda wote kuonana na watu anaowaongoza.

Hata hivyo, amesema kutokana na kushindwa kuwakutanisha watu pamoja na kuwafuturisha ameona atowe zawadi  kidogo japo hakusema ni nini kwa kuwa ni sadaka wapewe watu wenye uhitaji katika kila msikiti.

Ameongeza kuwa, amekua na utaratibu wa kutembelea wananchi na kufanya mikutano ya hadhara kusikiliza kero na kuzitatua au kuwasilisha sehemu husika iwe ni ngazi ya wilaya au ya juu zaidi kwa ajili ya kuitatua.

Mh Manota amesema kuwa yeye ni Kiongozi wa watu na muda wake wote atautumia kuwatumikia wananchi wa kimara iwe mchana au usiku yupo macho kwa ajili ya wananchi wa Kimara.

No comments:

Post a Comment