Mkurugenzi wa halmashauri ya Ilala akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salam leo mara baada kupokea msaada wa mapipa ya takataka yaliotolewa na Kamati ya Kina mama wa umoja wa Makanisa mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya halmashauri ya Ilala

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri(Kulia)akiweka vifaa vya Takataka Dar es Salaam leo Barabara ya Sokoine    mapipa hayo ya taka yametolewa na Kamati ya Kina Mama wa Umoja wa Makanisa Dar es Salaam,kwa ajili ya halmashauri ya Ilala

Manispaa ya Ilala wameendeleza zoezi la kuweka vifaa vya usafi katikati ya mji  ,vifaa hivyo vya takataka vimetolewa na Kamati ya Kina Mama ya Umoja wa Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam,(Pichani)Watumishi wa Manispaa ya Ilala Idara ya mazingira wakiwa wamebeba mapipa hayo ya Takataka(Picha ZOTE NA HERI SHAABAN)

NA HERI SHAABAN
MANISPAA ya Ilala imesema itaendelea kuwachukulia hatua wananchi wa Manispaa hiyo watakao chafua mazingira .


Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala Jumanne Shauri ,Dar es Salaam leo wakati wa mwendelezo wa kufunga vifaa vya kuifadhia takataka vilivyotolewa na Kamati ya Kina Mama wa Umoja wa Makanisa  Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya manispaa ya Ilala.


"Nawaomba wananchi wa Ilala muwe wa safi katika kutunza maeneo yenu  yote  msitupe takataka ovyo vifaa vya taka vipo maeneo yote kikubwa mzingatie tabia ya usafi"alisema Shauri.

Shauri alipongeza umoja wa makanisa wa mkoa huo kwa kupokea msaada huo wa vifaa vya taka  ili manispaa iweze kuwa safi.

Aliwataka wananchi kubadilika na kujenga tabia ya kuwa wasafi wakati wote   wasitupe taka ovyo waifadhi katika vifaa maalum

Akizungumzia oparesheni ya mifuko ya plastiki alisema katika manispaa hiyo wananchi wote wamewapa maelekezo mifuko ya plastiki wakabidhi kwa maofisa Watendaji wa Kata.

Kwa upande wake Mwenyekiti  wa Kamati ya Umoja wa makanisa Dar es Salaam Mchungaji Amani Lyimo alisema vifaa hivyo vya usafi thamani yake shilingi milioni 3.5.

Mchungaji Lyimo alisema umoja wao utaendelea kushirikiana na Serikali katika changamoto mbalimbali .

Naye Mkuu wa Idara ya kuhifadhi Mazingira na Taka Ngumu Ardom Mapunda alisema  jumla ya vituo 56 vimetengwa na halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa agizo la Serikali kukusanya mifuko ya plastiki .

Mapunda alisema mifuko hiyo inawasilisha katika ofisi za kata kisha zinapelekwa Ofisi ndogo ya halmashauri (Depo Kamata ) kwa ajili ya kuchukuliwa na Baraza la Hifadhi Mazingira (NEMC)
Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: