Thursday, 27 June 2019

KUTOKUWEPO KWA MAWAZIRI KWAKWAMISHA BUNGE LA BAJETI LA MAWAZIRI WA EALA KUENDELEA
Na Woinde Shizza  ,Arusha 

Mawaziri wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki(EALA) wamekwamisha mjadala wa bunge la bajeti la afrika mashariki baada ha kuto kuwepo katika kikao cha bunge hilo cha kujadili bajeti hiyo ya mwaka 2019/2020

Mawaziri  hao pamoja na manaibu wao ambao wapo 12  wanawakilisha nchi sita  zilizopo ndani ya Jumuiya ya Afrika madhariki ambazo ni Tanzania ,Kenya,Uganda ,Burundi,Rwanda  na Sudan kusini.

Wakiongea na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti walisema kuwa hawawezi kuendelea kujadili bajeti wakati mawaziri hao hawapo kwani haita kuwa na maana sababu mawaziri hao walitakiwa kuwepo na kusikiliza shida za wananchi wa Afrika mashariki zinazotolewa na wawakilishi wao ili waweze kutoa ufafanuzi  na ikishindikana wakazishughulikie baada ya bunge kumalizika

"tumeamua kwa umoja kugoma na kusema atutaingia bungeni kuendelea kujadili bajeti hii  wakati mawaziri ambao tulitaraji kuwauliza baadhi ya maswali ambayo yanahusu  bajeti hii ya mwaka 2019/2020 ,sasa tumeamua kutoendelea hadi pale mawaziri wote watakapo fika"alisema  Adamu Kimbisa 

Alisema kuwa taratibu za mabunge yote duniani zinajulikana na zinasema linapo jadiliwa bunge la bajeti katika mabunge lolote waziri husika alie wakilisha bajeti awepo .

"inashangaza tu kuona naibu waziri mmoja tu tena  kutoka nchini Burundi ndio yupo wengine wote hawapo na walitakiwa wawepo iliwaweze kusikia bunge hili kwani ni muhimu sana maana linaongelea mapato na matumizi katika mwaka wa fedha 2019/2020 "alisema Kimbisa


Kwa upande wake mwenyekiti wawabunge wa Tanzania bunge la jumuiya ya Afrika mashariki (EALA) Dkt. Abdallah Makame alisema kuwa jumuiya hii iliunda kwa lengo la ushirikiano na kuwaleta pamoja lakini mawaziri hawa wanavyokuwa hawaoni kani inavunja moyo wa kuwa na ushirikiano na sisi kama wabunge tunataka ushirikiano ,ushirikiano wa maneno ,ushirikiano  wa vitendo pamoja na ushirikiano katika hali na mali.

"napenda kusema atutaendelea na kikao chochote cha kujadili bajeti hii mpaka pale mawaziri hawa watakapo kuwepo"alisema Makame


Bunge hilo linaloendelea ndani ya makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliopo jiji Arusha limeairishwa  kwa siku mbili na linatarajiwa kuendelea apo kesho iwapo mawaziri wote watakuwepo.

940Picha mbunge wa Tanzania bunge la jumuiya ya Afrika mashariki (EALA)Adamu Kimbisa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya bunge hilo kuairishwa.

Wabunge wa jumuiya ya Afrika mashariki wakijadiliana nje ya jengo la ukumbi wa bunge la Jumuiya ya Afrika mashariki  mara baada ya kutoka katika kikao cha kujadili bajeti ya mwaka 2019/2020 inayoendelea kujadiliwa katika bunge hilo picha wa kwanza kulia ni mbunge wa bunge la Afrika mashariki (EALA)kutoka Tanzania Mariam Ussu pamoja na Pamela Masai

No comments:

Post a Comment