Sunday, 9 June 2019

KIGWANGALLA ASHIRIKI KUTOA TUZO KWA WAONGOZA WATALII BORA NCHINI

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Dkt. Hamisi Kigwangalla akifungua hafla ya utoaji wa Tuzo za Waongoza Watalii nchini (Tanzania Tour Guides Awards 2019) kwa mwaka ,jijini Arusha.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi tuzo ya Mwongoza Watalii Bora upande wa Wanaume, Bw. Athuman Njiku, wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa waongoza watalii jijini Arusha
 Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Mwenyekiti wa Kamati hiyo kwa upande wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe. Peter Msigwa, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akikabidhi tuzo kwa mshindi wa Waongoza Watalii Bora wa muda mrefu kwa upande wa wanaume.

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akiwapongeza Washindi wa Tuzo ya Waongoza Watalii Bora kwa mwaka 2019 kwa upande wa Wapagazi Wanawake. Wa pili kutoka kulia ni Jaji Mkuu wa mashindano ya Tuzo hizo Bw. Mozes Njowe kutoka Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori MWEKA.
 Majaji walioshiriki kuteua washindi wa Tuzo za waongoza Watalii kwa mwaka 2019 wakiwa katika  picha ya pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii mara baada ya utoaji wa tuzo hizo jijini Arusha.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi Tuzo ya mwongoza Watalii Bora wa muda mrefu Bi. Mary Mushi kwa kufanya kazi ya  kuongoza Watalii Mlima Kilimanjaro tangu mwaka 1979.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Kemilembe Walter akizungumza kwa niaba ya kamati hiyo wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo kwa waongoza watalii kwa mwaka 2019, jijini Arusha
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Kemilembe Walter akimkabidhi Tuzo ya Mwongoza Watalii Bora kwa upande wa Wanawake mwaka 2019, Rehema Otalu wakati wa hafla  ya utoaji wa Tuzo hizo  jijini Arusha.

No comments:

Post a Comment