kaimu mkurugenzi wa mwendeshaji wa kituo hicho cha mikutano  Victor Kamagenge akizungumza na waandishi

Na Woinde Shizza , Arusha 

Wafanyakazi wa kituo cha mikutano cha Arusha(AICC) kwakushirikiana na wafanyakazi wa baraza la utunzaji na usimamizi wa mazingira leo wamehitimisha kilele cha Wiki ya utumishi  Umma kwa kufanya usafi katika baadhi ya maeneo ya jiji  la Arusha ikiwepo hospital ya AICC inayomilikiwa na kituo .

Akiongea  na waandishi wa habari kaimu mkurugenzi wa mwendeshaji wa kituo hicho cha mikutano  Victor Kamagenge alisema kuwa katika wiki hii ya kuazimisha wiki ya watumishi wa umma wao kama kituo wamefanya kazi mbalimbali ikiwemo uongozi wa kituo kukutana na wateja wao waliopanga katika ofisi zao pamoja na Nyumba zao, wafanyakazi wa kituo hicho na wamehitimisha leo kwakufanya usafi katika hospital hiyo inaomilikiwa na kituo. 

Alisema kuwa lengo la kuazimisha siku hii kwakufanya usafi katika hospital hii ni kusaidia kuweka mazingira mazuri ya hali ya usafi katika hospital yao ambayo pia ni moja ya sehemu inayoingizia mapato kituo 

"mnajua tumeona tuje kufanya usafi hapa hospital ili mazingira yetu yazidi kuwa rafiki kwa wateja wanaokuja hapa kupata huduma, haiwezekani mgojwa anakuja hapa kutibiwa akimaliza anaondoka na ugonjwa mungine kutokana na mazingira kuwa machafu hivyo ndio maana tumekuja kufanya usafi "alisema Kamagenge

Alibainisha iwapo mazingira yatakuwa masafi na salama pamoja na huduma kuwa nzuri itasaidia ata wateja kuja kwa wingi na watapata fedha itakao saidia ata kupata gawiwo la serikali. 

Naye meneja  baraza la utunzaji na usimamizi wa mazingira (NEMC)kanda ya kaskazini Lewis Nzari Alisema kuwa wao kama wasimamizi  wamazingira wameamua kujiunga pamoja na kituo hichi kufanya usafi katika maeneo ya jamii kwani wanatambua kuwa mazingira yakiwa safi yanachangia kuhakikisha afya za watu zinakuwa nzuri. 

Aidha pia aliwapongeza wananchi wa mkoa wa Arusha na kanda ya kaskazini kwa ujumla kwa namna walivyopokea katazo la waziri mkuu Kasimu Majaliwa   la kuacha kutumia Mifuko ya plastiki ,kwani wananchi wamepokea kwa muitikio mkubwa. 

"mazara ya matumizi ya Mifuko ya plastick ni mengi sana kama vile uchafuzi wa mazingira, pia Mifuko hii inasababisha magonjwa  mengi kama vile kansa na magonjwa ya uzazi "alisema Nzari 

Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kupiga Vita matumizi haya ya Mifuko ya plasticki kwa kuwapa elimu wananchi wote ambao wanatumia pamoja na kuwakataza kutumia, maathimisho haya ya juma la utumishi wa uma yanafanyika kila mwaka na kauli mbiu ikiwa ni "kujenga Utamaduni wa utawala na matumizi ya tehama na ubunifu katika utoaji wa huduma jumuishi".




Picha baadhi ya wafanyakazi wa NEMC na AICC wakifanya usafi katika hospital ya AICC






Share To:

Post A Comment: