Monday, 10 June 2019

Halima Mdee atoka Hospitali, azungumza haya


Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amewashukuru wote kwa kumuombea na kutuma salamu za pole huku akisema ameshatoka Hospitali na afya yake ina imarika kwa kasi ya ajabu.

Halima amesema kuwa amesema hana cha kuwalipa kwa upendo Mkuu na awasimamie na kuwa bariki katika kila jambo mnalolifanya.

"Habari za asubuhi Wakuu. Kwa heshima kubwa, naomba niwashukuru wote kwa moambi na salamu za pole. Nimeshatoka Hospitali na afya yangu inaimarika kwa kasi ya ajabu. Sina cha kuwalipa kwa upendo wenu Mkuu, Mungu awasimamie na kuwabariki katika kila jambo mnalolifanya."

Halima alilazwa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam baada ya kufanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe tumboni.

No comments:

Post a Comment