Wednesday, 26 June 2019

CCM MKOA WA ARUSHA YAFANYA ZIARA YA KUKAGUZI WA MIRADI YA MAJI

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Loata Sanare akiwa pamoja na  Kamati ya Siasa ya Mkoa wakimsikiliza Mataalamu wa miradi ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya maji safi na maji taka Arusha (AUWSA) 
Ukaguzi wa Miradi ya Maji ukiendelea kama picha inavyoonekana 
Na.Vero Ignatus,Arusha.

Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha kimefanya ziara yake ya kukagua  miradi ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya maji safi na maji taka Arusha (AUWSA) na kuangalia  ubora na viwango vya miradi hiyo  ambapo wamewataka Wataalamu kuongeza kasi  ya utekelezaji ili kutatua kero ya maji kwa wananchi.

Loata Sanare ni Mwenyekiti wa CCM Arusha akiongozana na Kamati ya Siasa ya Mkoa pamoja na Wataalamu wakati akikagua miradi ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya maji safi na maji taka Arusha (AUWSA) ambapo amewataka Watendaji kuepuka matumizi mabaya ya fedha za miradi na kuisimamia vyema miradi hiyo ili iweze kuleta tija kwa wananchi.

Gabriel Daqqaro ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha amesema kuwa miradi hiyo ikikamilika inatarajia kuondoa kero ya maji katika jiji la Arusha kwa kuwa serikali imetenga fedha za kutosha kukamilisha miradi hiyo ili wananchi waweze kupata maji kwa asilimia 100.

Yasmin Bachu ni Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha   amesema kuwa miradi ya maji itasaidia kuwatua kinamama ndoo kichwani hususan wale waliokuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta huduma ya maji na kusumbuliwa na kero ya uhaba wa maji ambayo serikali imevalia njuaga kuitatua na kuimaliza.

Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halamashauri kuu ya CCM mkoa wa Arusha Robwrt Kaseko amepongeza Raisi Magufuli kwa juhudi zake za kuwatumikia Watanzania na kuwaletea maendeleo kwa kutenga fedha za kutosha kutatua kero ya maji kupitia miradi hiyo

Injinia Ruth Koya ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji  safi na Maji taka Arusha (AUWSA)  amesema kuwa miradi ya visima vinavyojengwa na kampuni za China inalenga kuhifadhi maji ya kutosha na kukabiliana na upungufu wa maji hivyo ujenzi ukikamilika
 jiji la Arusha litakua na maji ya kutosha.

Ziara ya Chama cha Mapinduzi imehitimishwa kwa kukagua miradi ya maji,madarasa ,hospitali ya wilaya pamoja na vituo vya afya lengo ni kuangalia utekelezaji wa ilani ya Chama hicho

No comments:

Post a Comment