Saturday, 22 June 2019

BREAKING NEWS : Elirehema Kaaya Ateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania(ALAT)


Mtaalam Elirehema Kaaya ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa(ALAT) na amekwisharipoti kwenye Ofisi za Jumuiya Hiyo zilizopo Jijini Dodoma.

Alipowasili Ofisini kwake mapema leo amekaribishwa na Mwenyekiti wa Alat Mhe. Gulamhafeez  Mukadam na kusema ana imani kuubwa na Kaaya pia ana uhakika atakwenda kuleta mabadiliko katika Jumuiya hiyo ambayo ina kazi kubwa ya kuziunganisha Halmashauri zote Nchini.

“Huyu ndio mtendaji Mkuu wa Jumuiya hii chini ya Usimamizi wangu ntampa ushirikiano wa kutosha ili Kazi ziende vizuri na Jumuiya yetu ipate mafanikio katika kuhudumia Halmashauri ambazo zinagusa kiuhalisia ndio zinazogusa maisha ya wananchi.

Naye Kaaya amesema ataitendea haki nafasi aliyopewa kwa kufanya kazi zinazoonekana na kuleta Taswira Njema wadau wa ndani na nje.

No comments:

Post a Comment