Afisa Utamaduni wa Manisp[aa ya Sumbwanga Kiheka Charles a.k.a K Chars. 
Katika kuunga mkono na kuieleza jamii juu ya juhudi zinazofanya nwa serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Dkt. John Pombe Magufuli, Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Sumbawanga Kiheka Charles a.k.a K Chars ameibuka na wimbo wa kuelezea mazuri yanayofanywa na serikali ya Tanzania.
Katika kueleza malengo ya kutunga wimbo huo alioupa jina la Mchaka Mchaka na kumshirikisha msanii Mackpaul Sekimanga a.k.a Makamua, K Chars alisema kuwa kama kiongozi na mshauri wa wasanii ni jukumu lake kuwaonesha wasanii mada mbalimbali za kuimba na sio kujikita kuyaimbia mapenzi wakati wanaweza kuimba kuhusu kuhamasisha lishe bora, kuhimiza kilimo cha mazao mbalimbali na faida zake, kukemea mimba za mashuleni, ndoa za utotoni, kuboresha huduma za afya nakadhalika.
"Hakuna msanii wa nje atakayekuja kusifu nchi yetu isipokuwa sisi wenyewe kusifia maendeleo yetu na kuyatangaza kwa wengine, hivyo nikaona niyaweke katika wimbo mazuri yaliyofanywa na serikali ambayo jamii inapaswa kuyafahamu, msanii ana nafasi kubwa ya kusikilizwa na jamii na yapo mengi ya kuyazungumzia katika maisha yetu, hivyo ni vyema wasanii wakajielekeza katika kuhamasisha mambo ya kimaendeleo, kuyaimba mazuri ya serikali na kuyaibua yale ambayo wanaona serikali inahitaji kuyafahamu ili yafanyiwe kazi," Alisema
Halikadhalika, alisifu juhudi za Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga, James Mtalitinya, kwa kumuunga mkono katika juhudi za kuibua vipaji vya wasanii wa Sumbawanga tangu kuanzishwa shindano la "Sumbawanga Talent Search" lililowahusisha wasanii wa kuimba, hadi kumalizika kwa shindano hilo.
Katika Shindalo hilo ambalo fainali yake ilifanyika usiku wa mkesha wa Mwenge wa Uhuru 2019 na mshindi wa kwanza alipata shilingi 300,000/=, wa pili 200,000/= na wa tatu 100,000/= na walioingia kwenye kumi bora wamepewa fursa ya kurekodi wimbo wa kuelezea fursa za uwekezaji zinazopatikana katika Mkoa wa Rukwa pamoja na kusifu ukarimu wa watu wa mkoa huo, kibao kinachotarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi July,2019.
K Chars ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi mbalimbali wa mkoa kuwasaidia na kuwaunga mkono wasanii wachanga wanaoutangaza mkoa.
Share To:

Post A Comment: