Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Khamis Mussa (katikati) akiwaonyesha waandishi kipeperushi cha maelezo ya ofa za mfungo wa Ramadhan zilizotolewa na kampuni ya Zantel kurahisisha mawasiliano na kupata taarifa mbalimbali za mfungo wakati wa uzinduzi wake uliofanyika mjini Zanzibar.Wengine pichani (kushoto ) ni Mkuu wa Bidhaa wa Zantel, Aneth Muga, na ( kulia ) ni Katibu wa Mufti za Zanzibar, Fadhil Soraga.
 Katibu wa Mufti za Zanzibar, Fadhil Soraga, akiongea katika mkutano wa waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofa za mfungo wa Ramadhan zilizotolewa na kampuni ya Zantel kurahisisha mawasiliano na kupata taarifa mbalimbali za mfungo wakati wa uzinduzi wake uliofanyika wiki hii mjini Zanzibar. Wengine pichani (kushoto) ni Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Khamis Baucha na (kulia) ni Mwanasheria Katika ofisi ya Mufti, Haji Habib Kombo.
Mkuu wa Bidhaa wa Zantel, Aneth Muga,akifafanua ofa hiyo katika mkutano wa waandishi wa habari ---

Kampuni ya mawasiliano ya Zantel, imezindua ofa maalum ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa wateja wake, ambayo itawawezesha kufanya mawasiliano kwa gharama nafuu sambamba na kupata taarifa muhimu kuhusiana na kipindi cha mfungo.

 Akitangaza ofa hiyo mjini Zanzibar, Afisa Mwandamizi wa Mawasiliano na Habari wa Zantel, Rukia Mtingwa alisema “Ramadhani ni muda muafaka wa kujenga mahusiano mazuri na ndugu, jamaa na marafiki, ofa hii ni ishara ya Zantel kuwasaidia wateja wake kuweza kuungana na kuwasiliana kwa urahisi zaidi na wapendwa wao na kupata taarifa muhimu za mwezi huu mtukufu”.

Mtingwa alisema ofa hii ya Ramadhani imelenga kuwazawadia wateja wa Zantel watakaojiunga na vifurushi mbalimbali vya muda wa maongezi vya siku, wiki na kifurushi cha mwezi. Wateja ambao wataweka kifurushi cha muda wa maongezi wa shilingi 999/- kila siku wataweza kupata jumbe za maneno za bure kati ya mtandao wa Zantel kwa Zantel, jumbe mbalimbali kuhusu mwezi wa Ramadhan, jumbe za kukumbusha wakati wa swala 5 na nukuu mbalimbali za maandiko ya Koran takatifu.

 Alisema wateja watakaoweka kifurushi cha wiki cha shilingi 4,999/ wataweza pia kupata jumbe za maneno za bure kati ya mtandao wa Zantel kwa Zantel, jumbe mbalimbali kuhusu mwezi wa Ramadhan, jumbe za kukumbusha wakati wa swala 5, kuwakumbusha muda wa kufuturu na nukuu mbalimbali za maandiko ya Koran takatifu.

 Hali kadhalika wateja wataoweka kifurushi cha mwezi cha shilingi 14,999/ wataweza kupata jumbe za maneno za bure kati ya mtandao wa Zantel kwa Zantel, jumbe mbalimbali kuhusu mwezi wa Ramadhan, jumbe za kukumbusha wakati wa swala 5, kuwafahamisha muda wa kufuturu na nukuu mbalimbali za maandiko ya Koran takatifu.

 Vifurushi vyote hivi vya Ramadhan vitapatikana kwa kujiunga kwa kupiga *149*15# na mteja anachagua aina ya kifurushi anachotaka kujiunga nacho.
Share To:

Post A Comment: