Saturday, 11 May 2019

Waziri wa mifugo atembelea kiwanda cha mazao ya mifugo Longido


Waziri wa mifugo na uvuvi mhe. Luaga Mpina amefanya ziara wilayani Longido Mkoani Arusha kukagua bwawa la kunyweshea ng'ombe pamoja na kiwanda cha nyama kiitwachwo elliya food overseas ltd.

Mhe . Mpina akiwa kwenye kiwanda hicho ameipongeza halmashauri ya Longido kwa kuamua kirekebisha majosho tisa na kuwa ahidi kurekebisha majosho mengine 8 yaliyo baki.

Sambamba na hayo mhe mpina ameuhakikishia uongozi wa kiwanda hicho kuwa serikali ya awamu ya ya tano inayo ongozwa na Dkt Magufuli kupitia wiazara yake umeanza kusimamia sheria na kuhakikisha kwamba nchi ya Tanzania haiwezia kugeuzwa kuwa dampo kwa ukiukwaji wa sheria za uingizwaji wa mazao ya mifugo itokayo nje ya nchi.

Kwa upande wake mmoja wa wa kutugenzi wa kiwanda hicho Bw Shabir Virji amesema kiwanda hicho kinatarajiwa kuanza uzalishaji mwezi wa 10 mwaka huu na kwa sasa wako katika hatua za ufungaji wa mashine katika kiwanda hicho.

Naye mmoja kati ya wafugaji katika wilaya ya Longido Bw Olekiande Sadala ameishukuru serikali ya awamu ya tano pamoja na mbunge wa jimbo hilo kwa kuweza kuwaletea kiwanda hicho wilayani humo na kusema sababu kubwa ya utoroshwaji wa mifugo kwenda nchi jirani ni ukosefu wa soko, kiwanda hicho kitaondoa tatizo la utoroshwaji wa mifugo walayani hapo.

Kiwanda hicho cha nyama kitawekewa jiwe la msingi na mbio za mwenge wa uhuru na kuzinduliwa rasmi mwezi wa 10 mwaka huu na kinatarajiwa kutoa ajira kwa watu takribani 200 na kwa siku kitakuwa na uwezo wa kuchinja Ng'ombe 500 pamoja na mbuzi 2000 kwa hatua za awali.

IMETOLEWA NA IDARA YA MAWASILIANO OFISI YA MKUU WA WILAYA YA LONGIDO
TAREHE 11-MAY-2019

No comments:

Post a Comment