Thursday, 30 May 2019

WAZIRI KAIRUKI AKUTANA NA WAWEKEZAJI WA UINGEREZA NCHINI

Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki akitoa neon la ufunguzi wakati wa mkutano wake na wawekezaji wa Uingereza nchini alipokutana nao Mei 29, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Coral Beach Jijini Dar es Salaam ili kujadili masuala ya uwekezaji nchini.
 Balozi wa Uingereza Nchini, Sarah Cooke akizungumza jambo wakati wa mkutano wa wawekezaji wa nchi hiyo walipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki alipokutana nao Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Anthony Mavunde akichangia jambo wakati wa mahojiano na waandishi wa habari walipokutana kujadili masuala ya wawekezaji nchini Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Waziri wa Nchi wa ofisi hiyo anayeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki na wa kwanza kushoto ni Balozi wa Uingereza Nchini Sarah Cooke.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) Oliver Vengula akichangia hoja wakati wa mkuatano huo.

Kamshina wa Kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Gabriel Malata akichangia hoja kuhusu vibali vya ajira wakati wa mkutano wa wawekezaji wa Uingereza uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa washiriki wa mkutano huo Russell Stuart akiuliza swali wakati wa Mkutano huo.

Kaimu Mkurugenzi wa Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu Aristides Mbwasi akijibu hoja za wajumbe kuhusu masuala ya uwekezaji wakati wa mkutano huo.

Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki akiteta jambo na Balozi wa Uingereza Nchine Sarah Cooke wakati wa mkutano huo.

Sehemu ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo.

Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) John Mnali akiwasilisha mada ya fursa za uwekezaji nchini wakati wa mkutano huo.

Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki  akiteta jambo na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira  Anthony Mavunde wakati wa Mkutano huo.

Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki  akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mahojiano kuhusu masuala ya uwekezaji nchini. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments:

Post a Comment