Friday, 31 May 2019

WAZIRI AZITAKA KAMPUNI ZUNAZOUNDA MAGARI YA UTALII KUFANYA KAZI KWA USHINDANI EPUKENI MIGOGORO ISIYO YA LAZIMA

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.George Kakunda,Satbir Hanspal Mkurugenzi wa kiwanda cha Hanspaul Mrisho Gambo Mkuu wa Mkoa wa Arusha 
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.George Kakunda,Satbir Hanspal Mkurugenzi wa kiwanda cha Hanspaul Mrisho Gambo Mkuu wa Mkoa wa Arusha 

Na.Vero Ignatus,Arusha
 Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.George Kakunda ametembela kiwanda cha kuunda bodi za magari ya utalii cha Hunspaul kilichopo njiro mkoani Arusha na kutoa maelekezo kwa Taasisi ya Brela na Tume ya Ushindani wa Kibiashara FCC kuangalia namna kampuni hizo na RSA ya Moshi zinazotengeneza magari ya utalii ili ziweze kufanya biashara zao kwa ushindani na kuepusha migogoro isiyo ya lazima

 Mhe Waziri ameyasema hayo leo ikia ni siku moja baada ya kutembelea  kiwanda cha RSA na kupokea malalamiko toka kwa wamiliki wa kiwanda hicho juu ya kuigwa kwa nembo yao ya kibiashara na moja ya kiwanda kilichopo mkoani Arusha.

"Ninaagiza BRELA na FCC waje hapa sio kwa lengo la kufunga kiwanda hiki ila ni kwaajili ya kuhakikisha kwamba utaratibu unawekwa vizuri ili uzalishaji wa Moshi uendelee na Uzalishaji wa Arusha uendelee na hiyo ndiyo kauli yangu ya mwisho kwani kiwanda hiki kimefanya uwekezaji mkubwa nawa kisasa na meshuhudia ubunifu mkubwa ikiwemo utenegenezaji wa magari yanayotumia umeme" alisema MheWaziri.

Satbir Hanspal Mkurugenzi wa kiwanda cha Hanspaul amemshukuru waziri wa viwanda na biashara kwa kutembelea kiwanda chao na kujionea uzalishaji unaoendelea,ambapo amesema wao kama wawekezaji wazawa wanajivunia serikali inayojali changamoto za wawekezaji kwani bado wana fursa kubwa ya uwekezaji nyumbani.

 Wawekezaji wazawa unajivunia sana kuwa na serikali inayojali changamoto za wawekezaji, Tanzania bado kuna fursa kubwa sana ya uwekezaji na sisi tumeamuakuwekeza nyumbani ndio maana pamoja na kiwanda hiki cha kutengeneza magari ya watalii tumefungua na kiwandakingine cha kutengeneza mifuko ya karatasi ili kutoa suluhisho baada ya serikali kupiga marufuku mifuko yaplastiki” alisema Satbir.

Mrisho Gambo Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambapo  amesema wao kama Serikali ya Mkoa wamejipanga kutoa ushirikiano kwawawekezaji wote walioko mkoani Arusha,amesema japo kuwa wanakumbana na changamoto za kibiashara lengo kuu ni kulinda chata zetu ndani kibiashara.

Sisi kama Mkoa tunajivunia sana uwekezaji huu na kuwepokwa kiwanda hiki Mkoani Arusha kwani ni sifa kwa mkoawetu na nchi kwa ujumlahivyo nipende kuwatia moyowawekezaji hawa wakati wowote wanapokumbana nachangamoto za kibiashara lengo letu ni kulinda brand zetu zandani” alisema Gambo.

Katika ziara hiyo  Mhe Waziri Kakundo aliweza kutembelea kiwanda cha Hanspaul Industries Liimites  kinachotengeneza mifuko ya karatasi kujionea uwekezaji mkubwa 
ambapo amewapongeza wawekezaji hao kwa kuweza kutafuta suluhisho  baada yakatazo la mifuko ya plastiki kuanzia tarehe 01 June 2019

No comments:

Post a Comment