Thursday, 30 May 2019

Wawili wafikishwa mahakamani kwa kumteka mtoto wa miaka 5Jeshi la Polisi mkoani Kagera limewafikisha watu wawili mbele ya Mahakama ya  Hakimu Mkazi Bukoba na kusomewa shitaka moja la kumteka mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitano (Jina linahifadhiwa) huko katika kijiji na cha brifani kata Kyaka wilaya ya Misenyi na kuanza kuwasiliana na baba yake mzazi wakishinikiza awape shilingi milion 15 ili waweze kumuachia.

Mwendesha mashitaka wa Serikali Haruna Shomari amewataja washitakiwa hao kuwa ni khalifa Hemed na Jonas Alphonce na ameieleza mahakama hiyo kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo May 13 mwaka huo.

Ambapo watuhumiwa hao walimvamia mtoto huyo alikuwa anatoka shule na kukaa naye kwa muda wa siku mbili hadi walipo kamatwa na jeshi la polisi.

No comments:

Post a Comment