Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Idd Kimanta.

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Wito umetolewa kwa wafugaji wa mkoa wa Arusha kuwa na vyama vya ushirika vya wafugaji wa ng'ombe wa Maziwa ili kujitengenezea wigo mkubwa wa kuweza kupata mikopo kutoka kwenye mabenki itakayowasaidia kujiendesha kibiashara.

 Iddi Kimanta ni mkuu wa wilaya ya Monduli ambapo amesema ukombozi mkubwa kwa nchi nzima kwa wafugaji wa ng'ombe wa maziwa ni kuwa na vyama ambapo  wafugaji wakifanikiwa kuwa na vyama vya ushirika watakuwa na uwezo mkubwa wa kukusanya maziwa na kupanga  namna ya kuweza kuuza 

Mhe.Kimanta amesema hayo wakati alipokaribishwa na bodi ya maziwa kutembelea mabanda ya maonyesho katika uwanja wa shekh Ameri Abed ambapo amesema amejifunza mengi kwa amewaona  wazalishaji wa  maziwa, bidhaa zitokanazo na maziwa pamoja na wafugaji wa ng'ombe wa maziwa. 

 Amesema wazalishaji wengi wa bishaa za maziwa  wanalalamika kuwa maziwa hayatoshi kwani uwezo wao wa kuzalisha bidhaani mkubwa kuliko upatikanaji wa maziwa yenyewe ili hali wazalishaji wa maziwa wanalalamika hawana masoko ya kuuzia maziwa.

"Mfano kiwanda cha Tanga Fresh kwa siku kinatakiwa kipate maziwa lita laki 120 lakini unakuta maziwa wanayoyapata pengine ni lita elfu 60 karibuni nusu ya uhitaji,Asas nao wanalalamika" alisema Kimanta
    
  Amesema bodi ya maziwa inatakiwa kuona ni wapi ambapo pamepungukiwa pia waangalie ni wapi penye tatizo ili waweze kupata ufumbuzi kwa pande hizi mbili zinazolalamika kati ya mzalishaji wa maziwa na muhitaji wa maziwa.  

Aidha ametoa shukrani  kwa baadhi ya mabenki walioshiriki katika maonyesho hayo CRDB na Tanzania Agricultural Bank ambapo amesema hao ni  wawezeshaji wakubwa wa wazalishaji na watengenezaji wa bidhaa za maziwa ilikuweza kuweka mnyororo wa bidhaa katika tasnia ya maziwa .         
  
Wiki hii ya Maziwa Kitaifa imebeba kauli mbiu isemayo Maziwa yaliyosindikwa kwa afya na uchumi wa viwanda ambapo ilizinduliwa juzi na Mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega na itahitimishwa tarehe mosi june ambapo mgeni anatazamiwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.  Luhaga Mpina.
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: