Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Iringa Lena Hongole akiongea kwenye kongamano hilo lilofanyika katika kijiji cha Kisinga' kata ya Kising'a lakini pia viongozi mbalimbali walishiriki kongamano hilo.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Daktari Abery Nyamahanga akitoa neno kwa UWT wakati wa kongamano la kumpongeza Rais Daktari John Joseph Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa.

Baadhi ya madiwani wa chama cha mapinduzi wakiwa wameshiriki katika kongamano hilo la UWT la kupongeza 
Rais Daktari John Joseph Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa.

Hii ndio ya pongezi iliyotolewa na UWT Iringa Dc kwa 
Rais Daktari John Joseph Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
 
Umoja wa wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Iringa wamefanya kongamano la kuunga mkono juhudi na kazi zinazofanywa na Rais Daktari John Joseph Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa.

Akizungumzia malengo ya kongamano hilo Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Iringa Lena Hongole amesema kuwa Rais amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo kwa wananchi waliomchagua 2015.

“Sisi wanawake wa wilaya ya Iringa tunampongeza sana Rais Daktari John Joseph Magufuli kwa kazi kubwa ya kuleta maendeleo wananchi waliomchagua kwa kipindi hiki kifupi tangu aingie madarakani”alisema Hongole

Hongole alisema kuwa Tanzania inakuwa kimaendeleo kwa kasi kubwa kutokana na uongozi wa Rais ambapo amefanikiwa kuwajenga watanzania kuwa wazalendo kwa kufanya kazi na kujituma kuhakikisha wanapata maendeleo.

“Mafanikio yenye tija tunayaona hivi sasa hivyo sisi kama wanawake hatuna haja ya kushindwa kumpongeza Rais wetu ambaye amekuwa kiungo muhimu cha maendeleo ya nchi hii hivi sasa” alisema Hongole

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Daktari Abery Nyamahanga amewapongeza wanawake hao kwa kuunga mkono juhudi za Rais.

“Nyinyi akina mama mmekuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi hizi ambazo zinazaa matunda ya kuleta maendeleo ndio maana tunaiona hata iringa inazidi kupata maendeleo kila kukicha tunaona sura mpya ya maendeleo ya nchi” alisema Nyamahanga

Nyamahanga alisema kuwa Rais Daktari John Joseph Magufuli amefanya mambo makubwa kwa kipindi kifupi kwa kuboresha sekta ya afya ,sekta ya elimu,uchumi,miundombinu  na utalii na kufanikisha maendeleo haya tunayoyaona hivi sasa.

“Hakuna mtanzania ambaye haoni nini kinafanyika katika nchi hii kwa kila mtu mwenye macho na masikio anajionea na kusikia maana hakuna ubishi kuwa Rais huyu amekuwa mzalendo kweli kweli katika nchi yetu hii” alisema Nyamahanga

Nyamahanga aliwataka wanawake hao UWT kukumbuka juu ya chaguzi zinazokuja hivi karibuni kuhakikisha wanakuwa na Wagombea ambao wanakubarika katika jamii ili kuhakikisha CCM wanashinda kwa kishindo.

“Wakina mama hakikisheni kama mnasifa ahakikisheni mnajitokeza kwa wingi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye chaguzi hizi zinazokuja na kuhakikisha tunamuunga mkono mgombea wa CCM na sio kutoka nje ya chama chetu” alisema Nyamahanga

Naye Diwani wa kata ya Kising’a Bi Ritta Mlagala amesema toka mwaka 2015 hadi sasa wamefakiwa kuboresha sekta ya afya na elimu kwa kutekeleza ilani ya CCM ya 2015 hadi 2020.

“Tumefanikiwa kujenga kituo cha afya,kuendelea kujenga majengo mapya ya shule ya sekondari ya Ilambilole iliyopo kata ya Kising’a na tumejenga madarasa manne na ofisi mbili katika shule msingi kising’a hivyo hayo ndio maendeleo yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano” alisema Mlagala

Aidha Mlagala alisema kuwa wameanza kujenga zahanati ya kijiji cha Mkungugu  na nyumba ya waaguzi ambazo zote zinatarajia kukamilika hizi karibuni licha ya kuwa na changamoto kadhaa ambazo zinatusukuma kuhakikisha tunatafuta wadau watuunge mkono kumalizia.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: