Monday, 13 May 2019

UVCCM WILAYA YA ARUSHA MJINI WAWAJIA JUU VIJANA WANAOTAPELI WAFANYABIASHARA.Katibu wa Umoja wa UVCCM Wilaya Arusha akizungumza na vyombo vya habari leo Ofisini kwake.

Mwenyekiti wa umoja wa was Vijana wa chama cha mapinduzi(Uvccm)wilaya ya Arusha Mjini akiwa na katibu wa Hamasa Abdi na Marijani na Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Mohamed Khalifa wakizungumza na Vyombo vya habari

Na.mwandishi wetu  -ARUSHA
Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Arusha Mjini umelaani vikali  baadhi ya vijana ambao wanajiita Viongozi wa Umoja huo kujipatia fedha isivyohalali kwa wafanyabiashara wa madini na wengine jijini Arusha.

Wakizungumza na waandishi wa habari Katibu wa Umoja huo Idd Ntonga alisema kuwa jambo hilo sio la kufumbiw macho kwa kuwa limekuwa likitia doa umoja huo.

Aidha alisema kuwa swala hilo linazidi kushika kasi kutokana na vitendo hivyo kukithiri na kupelekea wafanyabishara kutoa malalamiko yao pamoja na ushahidi kwakundi hilo.

“Pamoja na baadhi ya wafanyabiashara kuja kwetu na kulalamika ni kwamba tumeshachukua hatua kwa kupeleka majina ya wahusika katika vyombo vya sheria lakini pia tumeamua kuwaita waandishi wa habari ili pia kufahamisha umma wa watanzania juu ya utapeli huo ambao Uvccm hatuhusiki nao”alisema ntonga

Pia alisema kuwa chama cha mapinduzi kinaongozwa kwa taratibu  na kanuni mbali mbali ambapo amesema ikiwa kama kuna mchango wowote unahitajika upo utaratibu wa viongozi kufanya hivyo na sio kila mtu kujiendea kwa wafanyabiashara.

Kwa upande wake katibu Hamasa wa Uvccm wilaya ya Arusha Mjini Abdi Marijani  alisema kuwa pamoja na malalamiko hayo wapo baadhi ya vijana wamekuwa wakianzisha makundi katika mitandao wa (Whatsap) yenye jina la umoja huo ambao ameyataka kuacha mara moja.

Marijani  alisema kuwa Makundi hayo yamedaiwa kutumika vibaya kwa kuwaunga viongozi wakubwa wa serikali na kuwahoji badala ya kutumia vikao halali ambavyo vinatumika na chama hicho.

Nae mjumbe wa chama hicho Mohamed Kalifa amewatoa hofu wafanyabiashara jijini Arusha kuendelea na shughuli zao kwa kuwaserikali ya awamu ya tano imekuwa imeweka mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao.

Viongozi hao wamechukua hatua hiyo ya kuzungumza na vyombo vya habari  baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara kupeleka  malalamiko kwa viongozi wa chama hicho.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment