Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akikagua moja ya
gari lililoorodheshwa kwenye mkataba wa ujenzi kuwa ni tipa la tani 7
jambo ambalo ni kinyume na uhalisia.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako na wataalamu mbalimbali kutoka Chuo cha VETA taifa pamoja na Mkoa wakiangalia miongoni mwa matipa 11 yaliyoorodheshwa kwenye mkataba wa ujenzi baina ya Tender Internattional na Chuo Cha Ufundi VETa yakiwa hayafanyi kazi.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako na wataalamu mbalimbali kutoka Chuo cha VETA taifa pamoja na Mkoa wakiangalia miongoni mwa matipa 11 yaliyoorodheshwa kwenye mkataba wa ujenzi baina ya Tender Internattional na Chuo Cha Ufundi VETa yakiwa hayafanyi kazi.
Waziri wa Elimu nchini Prof. Joyce Ndalichako amethibisha
kuunda kamati itakayoshughulikia namna mkandarasi anayeendelea na ujenzi wa
chuo cha Ufundi Stadi (VETA) mkoani Rukwa alivyopata zabuni na kumtaka
mkandarasi huo ajieleze sababu zilizopelekea kuidanganya serikali katika
mkataba wake ulioonyesha uwepo wa vifaa vya kazi katika eneo la ujenzi huku
eneo hilo likiwa tupu na kazi zake kufanyika bila ya wataalamu na vifaa
vilivyoorodheshwa kwenye mkataba.
Ameongeza kuwa Kamati hiyo pia itashughulikia kuona endapo
thamani ya fedha iliyotolewa na serikali inaendana na majengo yaliyojengwa
katika eneo hilo ambalo yalitakiwa kujengwa majengo 22 ambapo hadi sasa ni
majengo 13 tu kikiwepo kibanda cha mlinzi ndio yameanza kuinuka. Wakati
mkandarasi hiyo akitakiwa kukabidhi majengo hayo mwezi Septemba 2019 hadi sasa
ujenzi huo umefikia asilimia 25 tofauti na makubaliano ya mkataba aliotakiwa
kufikia asilimia 61 hadi mwezi Mei.
Katika kuhakikisha wahusika wanashughulikiwa Prof Ndalichako
alimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa VETA nchini kuwachukulia hatua wale wote
waliohusika na kumuidhinisha mkandarasi (post qualification) aliyepewa zabuni pamoja
na kumtaka kumchukulia hatua Mkurugenzi wa VETA kanda ya nyanda za juu kusini
kwa kuonyesha kumtetea mkandarasi ambaye hana uwezo wa kazi.
“Wakandarasi wanaofanya kazi na Wizara ya Elimu badilikeni,
kwakweli miradi yangu yote nitaendelea kuipitia na nitaendelea kuchukua hatua
kali kwa wale wakandarasi ambao wanapata kazi kwa kiujanja ujanja, kwanza
nitashughulika na watu wangu wa kitengo cha manunuzi, hebu angalia vifaa kama
hivyo, kuna Afisa wa wizara ambae anapata mshahara ate serikali na alikwenda
akathibitisha akasema vifaa viko vizuri akaandika na ripoti, naoma Mkurugenzi Mkuu
anza na hao waliofanya “post qualification” kabla y ahata kamati haijaja
kufanya kazi wengine ambao watakumbwa sasa ni baada ya kamati kufanya kazi,
lakini Mkurugenzi wako wa Kanda hakufai kwasababu anaonekana yeye ni dalali wa
Mkandarasi” Alisisitiza.
Amesema hayo baada ya kutembelea ujenzi wa chuo cha ufundi Stadi
VETA katika eneo hilo la Kashai lililopo katika Manispaa ya Sumbawanga na
kuonyesha kutoridhishwa na kuelekeza kuwa kabla ya kuendelea na ujenzi huo lazima
vifaa vinavyotumika katika ujenzi vipimwe kuonyesha kama vinastahili ama
vinginevyo viondolewe katika eneo la ujenzi na mkandarasi huyo kuleta vifaa
vingine kwa gharama yake.
Awali wakati akisoma taarifa ya ujenzi wa chuo hicho Mkurugenzi
wa Kanda wa chuo cha VETA Justine Rutta alisema kuwa changamoto kubwa
iliyokuwapo ni mkandarasi huyo kucheleweshewa
malipo yake na hivyo anaidai serikali shilingi 51,039,153.59 hali
iliyosababisha kuchelewa kuendelea na ujenzi.
“Kwahiyo kwenye hela nayotakiwa kulipwa inaongezeka deni
hilo ambalo ni kwaajili ya kucheleweshewa ulipaji, hali ya malipo kwa mshauri
wa mradi, ameshalipwa tayari shilingi 1,051,144,000 tangu aanze kufanya kazi
hii na nyingine alitakiwa kulipwa mara atakapofikia hatua ya kuweka sakafu,
kwahiyo hatudai fedha yoyote mpaka sasa, changamoto katika mradi huu ndio kubwa
mradi umeweza kuchelewa kwasababu ya kuchelewa kulipwa kwa mkandarasi,”
alisema.
Katika hatua nyingine, Prof. Ndalichako alibaini uwepo wa
kampuni nyingine mbili zinazohusika na ujenzi wa chuo hicho, kampuni ambazo
serikali haikuingia nazo mkataba na baada yakuulizwa mhandisi wa ujenzi huo (site
engineer) aliyefahanmika kwa jina la Jin alisema kuwa kampuni hizo zilisaini
mkataba na Tender International kwaajili ya kuwapata vijana wa kufanya kazi,
kuwasimamia pamoja na kusimamia malipo ya vijana hao.
Prof. Ndalichako alisikitishwa na kitendo cha mkandarasi huyo
kuingia mikataba na kampuni nyingine ambazo hazikidhi viwango vya utekelezaji wa
miradi ya serikali kwani kati ya kampuni hizo moja inayoitwa Aricom Building
Constractors limited ilikuwa na daraja 7 na nyingine Laicom Building
Construcors ilikuwa na daraja 4. Na aliyagundua hayo baada ya kutaka kuonyesha
mikataba ya wafanyakazi wa ujenzi huo.
Tarehe
31/8/2019
mkandarasi Tender International alikabidhiwa kiwanja kwaajili ya kuanza
ujenzi
wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) katika Manispaa ya Sumbawanga ambapo
mshauri
Elekezi wa Mradi huo ni Sky Architect Consultancy Ltd na mradi huo
kutegemewa
kukamillika mwezi Septemba 2019 huku gharama za mradi huo ikiwa shilingi
10,700,488,940.05 na tarehe 22/11/2018 alilipwa shilingi
1,272,138,424.64. na tarehe 11/4/2019 alilipwa shilingi 835,598,299.01
na
kufanya jumla ya Shilingi 2,107,736,723.65 ya malipo kwa Mkandarasi huyo
ambayo ni sawa na asilimia 25 ya malipo yote.
Post A Comment: