Tuesday, 14 May 2019

TRA YATAKIWA KUIMARISHA UKAGUZI WA MASHINE ZA EFD


Na Ferdinand Shayo ,Arusha.

Mamlaka ya Mapato TRA mkoa wa Arusha imetakiwa kuimarisha ukaguzi wa mashine za  kielektroniki ili kuwabaini wafanyabiashara wanaokwepa kodi na kuikosesha serikali mapato ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua Kali za kisheria. 


Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro amesema hayo wakati akizindua wiki ya mlipa kodi iliyofanyika eneo la stendi kuu ya Mabasi ya mikoani,ambapo ameitaka TRA kuhakikisha kuwa wanakagua na kuwabaini wafanyabiashara wasiotoa risiti na kuikosesha serikali mapato jambo ambalo ni uhujumu uchumi.

Aidha amewataka Wafanyabiashara kutoa taarifa za siri juu ya baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wanaokwepa kodi ili hatua Kali zichukuliwe juu yao.

Kaimu Meneja wa TRA mkoa wa Arusha Irine Donald  amesema kuwa wataendelea kushirikiana n wafanyabiashara katika kutatua changamoto na kero zao ili waweze kufurahia kulipa kodi ya serikali.


Afisa Elimu kwa Walipakodi TRA Kanda ya Kaskazini Eugenia Mkumbo  amesema kuwa Mamlaka hiyo inatoa fursa kwa wafanyabiashara wanaolalamikia kukadiriwa kodi ya juu kuliko kipato chao.

Kwa upande wao wafanyabiashara Elisante Mungure na Winifrida Massawe Wafanyabiashara. wamelalamikia uwepo wa wamachinga mbele ya maduka yao huku wakiuza bidhaa zinazofanana hivyo kukosa soko la bidhaa zao.

No comments:

Post a Comment