MKUU wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza wakati wa wiki ya mlipa
kodi kwenye soko la Tangeru Mkoani Arusha
Kaimu Meneja
wa TRA Irene Donald akizungumza
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Mamlaka
ya mapato TRA mkoani Arusha imetoa onyo
kwa baadhi ya vishoka wanaowatapeli wafanyabiashara kupitia mgongo wa TRA waache
kufanya hivyo mara moja kwani watachukulia hatua kali za kisheria kwani
wanakwamisha ulipaji kodi kwa hiari.
Kaimu Meneja
wa TRA Irene Donald amesema hayo jana katika soko la Tengeru ambapo alizungumza na walipa
kodi katika wiki ya mlipa kodi ,ambapo amesema kuwa kuna baadhi ya watu
wanaofahamika kama vishoka ambao hufika TRA na kufanya udanganyifu kwa wafanyabiashara
kwa lengo la kujipatia faida huku wakiwaumiza wafanyabiashara.
Mkuu wa
Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amesema kuwa wafanyabiashara wanapaswa kulipa kodi
kwa hiari ili kuchangaia maendeleo ya nchi na kuiwezesha serikali kutekeleza
miradi ya maendeleo kwa wananchi wake.
Kwa upande
wao wafanyabiashara waliofika kupata
elimu ya mlipa kodi Magreth Pallangyo amelalamikia uchafu wa soko la tengeru
licha ya kulipa ushuru kwa Halmashauri hiyo hivyo wameiomba serikali itatue
changamoto hiyo ili waweze kulipa kodi stahiki.
Post A Comment: