MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati akikata utepe wakati wa sherehe ya ufunguzi wa soko la madini ya vito wilayani Mkinga kulia ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho kushoto ni Mkurugenzi wa madini wa shirika la Pact Cristina Villegas akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa uzinduzi huo kulia Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) (Tawoma) Eunice Negelo
 Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania  (Tawoma) Eunice Negelo
 Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo akizungumza  kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yona
 Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yona akizungumza kulia  Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo
 Mkurugenzi wa madini wa shirika la Pact Cristina Villegas akizungumza wakati wa ufunguzi huo ambapo aliipongeza Serikali ya awamu ya tano
 MENEJA wa (TRA) Mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza wakati wa ufunguzi huo
  Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo kushoto akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakati wa ufunguzi wa soko la Madini wilayani Mkinga kulia ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yonna
 Sehemu ya wadau wa madini na wachimbaji wakiwa kwenye ufunguzi huo
 Sehemu ya wadau wa madini na wachimbaji wakiwa kwenye ufunguzi huo
 Sehemu ya wadau wa madini na wachimbaji wakiwa kwenye ufunguzi huo
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akionyeshwa aina ya madini
Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo katikati akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia na Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yonna kushoto na kulia ni Katibu wa Tawoma Salma Kundi mara baada ya kufanya ufunguzi wa soko la madini wilayani humo
Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo kushoto akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negeloakiwa na Katibu wake kushoto Salma Kundi wakiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia na anayefiuatia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yonna
 Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo kushoto akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya sherehe ya ufunguzi wa soko la madini ya vito wilayani Mkinga .



MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella amesema Serikali itahakikisha inaendelea kuzipatia ufumbuzi wa kudumu changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo wadogo nchini ambazo zimekuwa ni kikwazo cha maendeleo yao

Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela wakati wa sherehe ya ufunguzi wa soko la madini ya vito wilayani Mkinga .

Alisema kuwa licha ya wachimbaji hao kufanya kazi nzuri ya uchmbaji lakini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo uduni wa vifaa ,masoko pamoja na mitaji .

“Ufunguzi wa soko hili ni kielelezo cha kuonyesha namna ambavyo serikali yenu ipo tayari katika kuanza kushughulikia changamoto zenu kwani uwepo wa soko hili tayari ni mkombozi kwenu”alisema Mkuu wa mkoa huyo.

Alisema kuwa changamoto nyingine ni namna ambavyo wataweza kuongeza thamani madini hayo ili yaweze kupata soko la uhakika na kwa haraka.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo alisema kuwa uwepo wa soko hilo utasaidia kudhibiti utoroshwaji wa madini.

Vile vile alisema kuwa uwepo wa soko hilo utaweza kuwasaidia wachimbaji wadogo kupata fursa ya masoko ambapo hapo awali ilikuwa ni changamoto kubwa kwao.

“Tunaimani sasa serikali itaweza kupata mapato yake vizuri na wachimbaji wataweza kuuza madini yao kwa uhakika bila ya hofu ya kuweza kutapeliwa na wajanja wachache”alisema Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho alisema kuwa soko hilo ndilo ambalo litaweza kutoa dira ya uanzishaji wa masoko mengine mkoani humo.

Alisema kuwa mkoa huo unautajiri wa madini lakini wachimbaji wadogo waliowengi walikuwa hajaweza kunufaika biashara hiyo kutokana na ukosefu wa masoko ya uhakika.

Mkurugenzi wa madini wa shirika la Pact Cristina Villegas aliipongeza serikali kwa kuja na uamuzi wa masoko hayo kwani utasaidia kuzui utoroshwaji wa madini kwa kiasi kikubwa.

“kwa uwamuzi wa serikali utasaidia kudhibiti mapato yake lakini na mchimbaji mdogo ataweza kuona manufaa ya shughuli ya uchimbaji anayoifanya’alisema Villegas.

MWISHO
Share To:

Post A Comment: