Kijana Salum Ramadhan Salum (18) amepotea,  hakurejea nyumbani tangu tarehe 12th May 2019. 

Mara ya mwisho ameonekana stendi ya Ukonga madafu akipanda gari ya kutoka Gongo la Mboto likielekea buguruni ikiwa ni safari yake ya kurejea nyumbani majira ya saa 2 usiku.

 Alikuwa amevaa shati jeupe na Suruali ya kijivu na saa rangi ya dhahabu na sendoz za wazi. 

Tafadhali toa taarifa kituo cha polisi kilicho karibu na wewe au naomba unijulishe kwa kupiga ama kuandika sms kwenda nda namba 0713/0766-202748. 

Aliyepotea ni shemeji yangu kabisa na mimi ndiye mlezi wake. 

Ni kijana mpole na mwenyeji wa Kiwalani BomBom kwa DSM na Mwanza ndio alipozaliwa. 

Picha zake ni kama unavyoweza kuona viambatanisho vya ujumbe huu.

Naaomba Ushirikiano wenu kwenye changamoto hii.
 
Asante

Share To:

msumbanews

Post A Comment: