Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo amezindua Soko la madini Wilayani Longido ikiwa ni sehemu ya maagizo yaliyo tolewa na mh. Rais wa Jamuhuri ya muungano ya Tanzania John Pombe Magufuli.

RC Gambo amesema sifa zinazo pelekea uwepo wa soko la madini ni uwepo wa usalama wa uhakika, uwepo wa uhamiaji, uwepo wa benki na TRA pamoja na maafisa wa madini.

Aidha RC gambo amesema soko hilo la madini la Namanga wilayani longido litaondoa adha mbalimbali kwa wafanyabiashara wa madini ikiwemo ile ya utapeli, utoroshwaji wa madini pamoja na ujanja ujanja.

Sambamba na hayo pia mh. Gambo amewasii wafanyabiashara wa madini Mkoani Arusha pale wanapo kutana na changamoto mbalimbali katika soko hilo wawasiliane na Ofisi ya Mkuu wa wilaya, wawasiliane na ofisi yake ya mkuu wa mkoa pamoja na ofisi zote za Serikali.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe amemshukuru mh. Rais Dkt John Magufuli kwa kusikiliza kero za wafanyabiashara wa madini na kuwaondolea tozo mbalimbali zilizo kuwa kero kwa wafanyabiashara hao.

Sambamba na hayo pia mwaisumbe amewataka wafanyabiashara hao kulitumia soko hilo kwani soko hilo ni la kwao na wala sio la Serikali hivyo basi walitumie vizuri.

Nae Mwenyekiti wa taifa wa wachimbaji madini bw. salama rea amempongeza Rais Magufuli kwa kuakikisha mabadiliko ya mswada ya mabadiliko ya ongezeko la dhamani pamoja na kodi ya zuio kufutwa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: