Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole akizungumza wakati wa semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akifuatiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
 Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole wa pili kutoka kushoto akisisitiza jambo wakati wa harambee hiyo kulia ni katibu wa CCM wilaya ya Tanga Salim Kidima ambaye amshikilia fedha zilizochangishwa kwenye harambee hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba
 MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akiwa kwenye haraambee hiyo kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Tanga Salim Kidima akiwa anahesabu fedha zilizotolewa

 Sehemu ya wanachama wa CCM wilaya ya Tanga wakifuaatilia kwa umakini hotuba ya Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole wakati wa semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu



WANACHAMA wa chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga wametakiwa kujenga mshikamano na umoja miongoni mwao ili kuweza kuhakikisha wanakiwezesha chama hicho kupata ushindi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani

Hayo yalisemwa  na Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole wakati wa semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu

Alisema lazima kuwepo mshikamano ambao utaawasaidia kuweza kuhakikisha wana kuwa wamoja kuelekea kwenye chaguzi zijazo ili kuhakikisha chama hicho kinaendelea kuwatumikia watanzania kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.

Aidha pia katika harambee hiyo Katibu huyo alifanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Tanga ambapo jumla ya shilingi milioni 18 ziliweza kupatikana papo kwa papo huku Mbunge wa Viti Malumu (CCM) Mkoani Tanga ambaye pia Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akichangia shilingi milioni 5.

Sambamba na uchangiaji huyo lakini Waziri Ummy alitoa pia bendera za mashina 1000 na sare za chama ili kuimarisha chama ngazi za chini huku bendera 1000 za mabalozi na tisheti 800 ambazo watazitumia kwenye shughuli mbalimbali za kichama .

Hata hivyo Katibu huyo alitembelea eneo la Masiwani kutakapojengwa ofisi mpya ya CCM wilaya ya Tanga pia alihimiza mshikamano na upenda kwa wana CCM ili kuweza kuhakikishaa wanapiga hatua kubwa za kimaendeleo.

Share To:

Post A Comment: