Tume ya Taifa ya chaguzi inapenda kuutaarifu Umma kuwa, haihusiki na matangazo ya nafasi za ajira yaliyobandikwa katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
 
Matangazo hayo yanaeleza kuwa, Tume imetoa ajira za muda, na wananchi walioomba ajira hizo wamekuwa wakiambiwa watoe kiasi cha fedha kwa madai kuwa ni kwa ajili ya mafunzo.
 
Hatua kali za Kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu au kundi la watu wanaotumia au wanaopanga kutumia jina la Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufanya vitendo vya kihalifu.
 
Tunapenda kuwashukuru wananchi na kuwasihi kuendelea kutoa taarifa mara tu wanapohisi uwepo wa watu au kundi la watu wenye nia mbaya ya kulichafua jina la Tume yaTaifa yaUchaguzi.
 
Dkt. Athumani Kihamia
MKURUGENZI WA UCHAGUZI
Share To:

msumbanews

Post A Comment: