Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema inasubiri nakala ya hukumu ya mahakama kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) iliyobatilisha kifungu cha Sheria ya Uchaguzi Namba 7(1) na 7(3) kinachowaruhusu wakurugenzi wa halmashauri kusimamia uchaguzi, ndipo ijue cha kufanya.

Hapo juzi Mahakama Kuu ya Tanzania imebatilisha sheria inayowapa mamlaka Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia Uchaguzi Mkuu kwa sababu wanateuliwa na Rais na hawapo katika mfumo wa Tume Huru.

Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Atuganile Ngwala kwenye kesi ya msingi namba 6 ya mwaka 2018 iliyofunguliwa na mtoto wa marehemu Chacha Wangwe ambaye ni Bob Chacha Wangwe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Share To:

msumbanews

Post A Comment: