Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa UNICEF nchini Bi. Maniza Zaman ambaye amemaliza muda wake alipomtembelea Ofisi kwake iliyopo Jijini Dodoma.

 Katika mazungumzo yao, Mhe. Mavunde amelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa la UNICEF kwa kushirikiana na Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo na kwa kutoa misaada katika sekta mbalimbali nchini.

 “UNICEF imekuwa ikishirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu katika masuala mbalimbali yaliyolenga kuboresha na kuimarisha utekelezaji wa Sera ya Hifadhi ya Jamii (Social Security Policy of 2003), kuwapatia mafunzo watumishi katika masuala ya virutubishi na hifadhi ya jamii, pia kuwapatia vitendea kazi kama vile komputa na magari ambayo yanatumika kwenye miradi mbalimbali,” alieleza Mavunde.  

 Aliongeza kuwa, Serikali imeguswa na jitihada za UNICEF na itaendeleza ushirikiano na shirika hilo katika kutekeleza jukumu la kuhudumia Watoto.

 Aidha, Naibu Waziri Mavunde alimpongeza Bi. Maniza Zaman kwa kazi nzuri aliyofanya kipindi cha muda wake na kumsihi kuendelea kuwa balozi mzuri wa masuala ya Watoto.
 “Tutakukumbuka kwa juhudi na ushauri uliokuwa ukitupatia katika masuala ya elimu na haki za Watoto,” alisema Mavunde.  

 Kwa upande wake, Bi. Maniza Zaman amesema anaishukuru Serikali kwa ushirikiano iliompatia kwa kipindi chote alichokuwa hapa nchini.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akijadili jambo na Mkuu wa Ushauri na Sera za Kijamii Bw. Paul Van Lifford (kulia), (katikati) ni Mkurugenzi wa Hifadhi ya Jamii Bw. Daud Kaali.
Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Bi. Maniza Zaman (kulia) akimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde. (katikati) ni Bi. Khadija Othman mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Bi. Maniza Zaman, akimweleza jambo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavundealipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma. (Kulia) ni Bi. Khadija Othman mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 Mkuu wa Ushauri na Sera za Kijamii Bw. Paul Van Lifford (kushoto), akieleza jambo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (kulia) kuhusu ushirikiano baina ya UNICEF na Serikali katika utekelezaji wa Sera ya Hifadhi ya Jamii (Social Security Policy).
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akijadili jambo Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Bi. Maniza Zaman, mara baada ya mazungumzo yao, Jijini Dodoma.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: