Serikali imesema watumishi wa umma hawapaswi kuomba nyongeza ya mwaka ya mshahara, bali Serikali ndiyo yenye uamuzi wa kutoa au kutotoa nyongeza.

Hayo yamesemwa bungeni leo Mei 14, na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na utawala bora) Dk. Mary Mwanjelwa wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Tunza Issa Malapo (Chadema).

Mbunge huyo alitaka kujua serikali inatumia sheria ipi kutowapa wafanyakazi stahiki zao zinazohusu kupandishwa madaraja, na ongezeko la mwaka.

Katika majibu yake, Dk. Mwanjelwa amesema kwa mujibu wa kanuni E.9 (1) ya kanuni ya kudumu katika utumishi wa umma za mwaka 2009, toleo la tatu, nyongeza ya mwaka ya mishahara haipaswi kuombwa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: