Wednesday, 8 May 2019

MANISPAA YA ILALA KUTENGA KITUO CHA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI

 Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto(Katikati) akiangalia bidhaa za Wajasiriamali wa Wilaya ya Ilala  katika uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Segerea (Picha na Heri Shaaban)
 Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbila moto  akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Segerea Dar es salaam leo(kushoto)Ofisa maendeleo Manispaa ya Ilala Fransica Makoye(kushoto) Mwenyekiti wa Jukwaa wa kata ya segerea Julieth Banigwa(Picha na Heri Shaaban)
 Katibu wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoa Dar es Salaam Husna Shechonge akiongea katika uzinduzi wa Jukwaa segerea (NA.HERI SHAABAN)
Mratibu wa Dawati la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Wilaya ya Ilala Georgis ASENGA akizungunza na katika uzinduzi wa Jukwaa kata ya Segerea (Picha na Heri Shaaban)

NA HERI SHABAN
MANISPAA ya Ilala  imesema inatarajia kutenga eneo la Mnazi Mmoja kwa ajili ya Biashara za Wajasiriamali.

Hayo yalisemwa na Kaimu Meya wa Manispaaa ya Ilala Omary Kumbilamoto wakati wa kuzindua Jukwaa la Wanawake la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi  Kata ya Segerea Wilayani Ilala Dar es salaam .

"Manispaa yangu ya Ilala imetenga eneo la uwanja mdogo Mnazi Mmoja litatumika kwa ajili ya bidhaa mbalimbali za Wanawake pamoja na eneo la Ocen road Wajasiriamali wa Wilaya ya Ilala watakuwa wanauza biashara zao" alisema Kumbilamoto.

Aidha alisema Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa Kushirikiana na Mkurugenzi wa halmashauri wanaweka utaratibu mzuri kuboresha eneo hilo ili liwe sehemu ya kutuo cha biashara kwa wilaya ya Ilala.

Kumbilamoto aliwataka Wanawake kuchangamkia fursa kujikwamua kiuchumi kila mtu ajishughulishe
.
Alisema Manispaa ya Ilala inatarajia kutoa mikopo awamu ya tatu Mei 30 mwaka huu dhumuni kila mtu aweze kupata mikopo hiyo akuna riba wala kizuiz.

"Halmashauri yetu imejipanga vizuri inatarajia kutoa mikopo shilingi bilioni 2 wananchi wa Manispaa ya Ilala wacha kusikiliza radio mbao fedha zipo  bila riba "alisema.

Kwa upande wake Katibu wa Jukwaa Mkoa Dar es Salaam Husna Shechonge alisema  Majukwaa ya Wanawake hayana fedha dhumuni lake kutambua nafasi zetu tulizonazo .

Husna alisema majukwaa ya wanawake yote ameadhishwa sio kwa ajili ya dhumuni la mikopo majukwaa ya uwezeshaji Wanawake Kiuchumi hayana mikopo.

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi kata ya Segerea Julieth Banigwa alisema  jukwaa la Segerea lina vikundi 17 vya Wajasiriamali vilivyosajiliwa na vingine vipo katika hatua za usajili .

Banigwa alisema jukwaa hilo limewawezesha kutengeneza mtandao wa biashara ambapo imewasaidia kupanua wigo wa masoko na bidhaa zinazozalishwa katika vikundi.
Akielezea changamoto alisema wana vikundi kutokuwa na elimu ya ufungashaji na udhibiti wa ubora .
Pia ukosefu wa masoko ya uhakika ya bidhaa zinazozalishwa na wana Jukwaa katika vikundi.
Mwisho

No comments:

Post a comment