Friday, 31 May 2019

MALEMBEKA NA GURU PLANET KUTOA MAFUNZO KASKAZINI UNGUJA


NA HERI SHAABAN

Mbunge Wa Viti Maalum Kaskazini Unguja, Mhe. Angelina Malembeka ameandaa na kudhamini mafunzo ya ujasiriamali na elimu ya mikopo kwa wanawake wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 Mafunzo yatatolewa na kampuni ya Guru Planet yatafanyika siku ya Jumamosi tarehe 1 juni eneo la Mahonda katika ukumbi wa CCM ,Mkoa wa  Kaskazini Unguja


Malembeka alisema mafunzo hayo yanatarajia kuanza kuanzia saa 4.00  asubuhi. Mafunzo hayo ya siku moja yatafunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mhe. Thuwaiba Kisasi.

"Nimeandaa mafunzo ya Ujasiriamali sambamba na utoaji elimu ya mikopo mafunzo hayo yatafunguliwa na mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti UWT Thuwaiba Kisai  kufungwa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu CCM, Komred Kimea (Mnec)alisema Malembeka.

Aidha aliwataka wanawake kujikwamua kiuchumi na kuacha maisha tegemezi aliwataka wajiendeleze katika kufahamu elimu ya ujasiriamali ili  waweze kujiendeleza .


Aliwataka wanawake navijana kutumia fursa hiyo katika kujishugulisha ili waweze kujiongezea kipato.

Mwisho

No comments:

Post a Comment