Thursday, 30 May 2019

Lazaro Nyalandu afunguka mwanzo mwisho kuhusu kukamatwa kwakeWaziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ameelezea tukio zima la kukamatwa kwake na Jeshi la Polisi mkoani Singida na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Kupiti ukurasa wake wa Instagram ameeleza hilo;,

Nawashukuru sana WOTE walioguswa na MKASA ulionisibu katika saa ya kujaribiwa kwangu mnamo majira ya 8:30 mchana Jumatatu, tarehe 27 Mei 2019. ASANTENI SANA. 
Tuliwasili kijijini Itaja, Wilayani Singida kuongea na VIONGOZI wa vijiji na vitongoji Kata ya Itaja kuhusu zoezi linaloendelea nchi nzima la chama chetu CHADEMA kuwatambua na kuwaandikisha wanachama wetu. Jumla ya washiriki walioorodheshwa katika daftari la mahudhurio siku hiyo walikua watu 29.

Kama ilivyoripotiwa, kikao chetu cha NDANI, kilivamiwa na watu ambao hatukuwafahamu, wakiwa na silaha na kuamrisha mimi, pamoja wenzangu wawili (David Jumbe na Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Itaja, ndugu Peter) tuondoke nao.

SOTE tulipatwa na mshtuko mkubwa, na hatukupewa utambulisho wala sababu ya kutolewa kwenye kikao na kuchukuliwa na watu wenye silaha mithili ya wahalifu na kutiwa nguvuni, huku wote tuliokuwa nao wakiwa wamepigwa bumbuwazi.

Walimchukua kila moja wetu katika chumba tofauti na kutuhoji juu ya UHALALI wa Kikao hicho cha CHADEMA, na kudai kuwa kulikuwa na HARUFU ya rushwa. Baada ya mahojiano, walitupeleka katika kituo kikuu cha Polisi Singida, na muda mfupi baadae tukasikia taarifa ya TAKUKURU Singida kuwa wao wamejiridhisha hapakuwa na tatizo na wametukabidhi mamlaka ya Polisi.

Polisi walitufanyia mahojiano mengine, kila mmoja wetu katika chumba tofauti, na kutujulisha kuwa wao hawakuwa na neno lolote juu yetu, isipokuwa yatupasa tutoe taarifa kwa OCD Singida. Tulipopewa dhamana usiku huo, ilikuja AMRI KUTOKA JUU kwamba dhamana hiyo ifutwe, na tukalazwa katika rumande ya Central Police.

UONEVU ni dhambi mbele za Mungu, na wanadamu. CHADEMA na Vyama vingine vyote vya Upinzani wamewekwa katika hali ya mashaka na mateso, na tunatishiwa usalama wetu, na kuwekewa mipango LUKUKI ya kututungia na KUTUBAMBIKIZIA kesi. Hakika, HAKI huinua TAIFA, na WOTE wenye MAMLAKA, waone fahari kutenda MEMA. Kwa nilichokipitia siku hizi chache, nawasihi sana CHADEMA, na UPINZANI kwa ujumla wake, SIKU tutakapo shinda na kushika DOLA, tusiwafanyie wana CCM au watu wengine mateso kama haya, kwakuwa, yatupasa tuushinde UBAYA kwa WEMA.

No comments:

Post a Comment