Monday, 13 May 2019

Kisa mvua, UDA-RT yasitisha usafiri wa mabasi ya mwendokasiKampuni ya UDA-RT imesitisha huduma zake katika njia ya Kimara-Kivukoni, Kimara-Gerezani, Morroco-Kivukoni na Morroco-Gerezani kuanzia saa 10:30 alfajiri leo.

Huduma zinazotolewa kwa sasa ni kati ya Kimara-Mbezi, Kimara-Magomeni Mapipa, Kimara-Morroco, Gerezani-Muhimbili, Kivukoni-Muhimbili na Gerezani-Kivukoni.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano UDA-RT, Deus Bugaywa imeeleza kuwa wanaendelea kufuatilia hali ya maji katika eneo husika, maji yakipungua huduma zitarejea katika hali ya kawaida.

No comments:

Post a Comment