Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere akizungumza
Na
Ferdinand Shayo,Arusha.
Kamishna
Mkuu wa Tra, Charles Kichere amefanya
ziara ya kutembelea maduka jijini Arusha
na kutoa elimu kwa wafanyabiashara ikiwemo kukagua mashine za
kielektroiniki pamoja na kusikiliza changamoto za wafanyabiashara hao na
kuzipatia ufumbuzi.
Kichere amefika
katika maduka mbalimbali yaliyopo jijini Arusha na kuzungumza na
wafanyabiashara hao ana kwa ana ikiwa ni mpango wa kuwafikia wafanyabiashara na
kuwasikiliza katika wiki ya elimu kwa mlipa kodi innayoendelea mkoani Arusha.
Aidha
amewataka wafanyabiashara hao kushirikiana bega kwa began a mamlaka hiyo na
kulipa kodi kwa hiyari ili kuchangia maendeo ya taifa .
Kamishna
huyo ametembelea soko la Ngaramtoni na kuzungumza na Wafanyabiashara ambao
walitoa kero zao na kuzitolea majibu ikiwa ni utekelezaji wa dhana ya kutoa
elimu kwa walipa kodi.
Kwa Upande
wake Mfanyabiashara Swalehe Mkwizu ametoa mapendekezo yake ya kuitaka Tra
iongeze wigo wa kukusanya kodi katika vyanzo vipya ili kuongeza mapato badala
ya kutegemea vyanzo vilivyopo
Salehe
amesema kuwa kwa sasa TRA inafanya kazi nzuri ya kuhakikisha kuwa inawahudumia
vyema wafanyabiashara kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa hivyo kupunguza
msongamano wa watu katika ofisi zao.
Mfanyabiashara
wa Duka la Pembejeo Godlisten Jackson ameiomba TRA uwapunguzie kodi kutokana na
mlolongo wa kodi walizonazo kutoka katika mamalaka nyingine ili waweze kufanya
biashara hiyo na kuleta tija.
Post A Comment: