Kada wa CHADEMA, Bob Chacha Wangwe ameeleza ni kwanini alienda mahakamani kupinga wakurugenzi wa Halmashauri kuwa wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu.

Akizungumza leo na kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV ameeleza kuwa alifanya hivyo ili sheria ifutwe na itungwe sheria ambayo haitafungamana na vyama vya siasa.

"Ibara ya 74 inakataza msimamizi wa uchaguzi kujiunga na chama chochote cha siasa, msimamizi akiwa mwanachama wa chama chochote cha siasa atakuwa na maslahi na chama hicho, kwahiyo uchaguzi hautakuwa huru na haki, tunaona wasimamizi wa uchaguzi wanavaa hadi 'uniform' za vyama vya siasa," ameeleza.

"Kabla ya kufungua kesi hii tulifĂ nya utafiti tulibaini wakurugenzi 74 ni makada wa Chama cha
Siasa, tena walikuwa ni makada wa wazi, wengine tunawajua na wengine walishawahi kugombea nafasi za uongozi kwenye chama," amesema Wangwe.

Utakumbuka Mei 10 mwaka huu Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, ilitoa uamuzi kuhusu Shauri la Kikatiba namba 17 la mwaka 2018 lililofunguliwa na Bob Chacha Wangwe kupinga baadhi ya vifungu vua Sheria ya Taifa ya Uchaguzi vinavyohusu Wasimamizi wa Uchaguzi kuwa vinakinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho.

 Shauri hilo lilifunguliwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Taifa yaUchaguzi na Mkurugenzi wa Uchaguzi.

Hata hivyo, hapo jana Serikali imewasilisha notisi Mahakama ya Rufaa kupinga sehemu ya uamuzi wa Mahakama Kuu katika kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Bob Chacha Wangwe dhidi Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wenzake kupinga baadhi ya vifungu vya Sheria ya Taifa Uchaguzi kuhusu Wasimamizi wa Uchaguzi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: