Maafisa na Askari wa jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), wanaoshiriki Ulinzi wa Amani katika  Jimbo la Darfur nchini Sudan kwa Mara ya kwanza  kwa kipindi cha Miaka 10 ya Ulinzi wa Amani Jimboni humo wametumia Ndege ya Shirika la Ndege ya  Serikali ya Air Tanzania.

Wamefanya hivyo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu katika  kulifanya Shirika hilo linapiga hatua zaidi kwa maslahi ya Shirika na Taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita wa JWTZ Meja Jenerali Alfred Kapinga Akiagana na  Maafisa na Askari wa  JWTZ Kundi la 13 linalokwenda kushiriki Ulinzi wa Amani Jimboni Darfur Nchini Sudan wakati wakiondoka kwa Ndege ya ATCL Mei 16  katika Uwanja wa Ndege wa Jeshi Jijini Dar.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: