Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebosi akisisitiza jambo wakati wa kikao cha baraza la Madiwani cha kuwasilisha taarifa ya utendaji wa kata kulia ni
Kaimu Mkurugenzi Ramadhani Possi
 Kaimu Mkurugenzi Ramadhani Possi akizungumza wakati wa kikao hicho
 Diwani wa Kata ya Maweni Jijini Tanga Calvas akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Diwani wa Kata ya Pongwe Mbaraka Sadi
 DIWANI wa Kata ya Mswambweni (CUF) Abdulrahamani  akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Diwani wa Kata ya Chumbageni (CCM) Saida Gadafi
 Baadhi ya madiwani wakipitia makabrasha wakati wa kikao hicho
HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imeeleza namna vitambulisho vya wajasiriamali vilivyotolewa na Rais John Magufuli vilivyowasababishia kukosa mapato huku vyanzo vyake vya mapato 15 kufutika na hivyo kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo.
Kauli hiyo aliitoa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebosi wakati wa kikao cha baraza la Madiwani cha kuwasilisha taarifa ya utendaji wa kata kilichofanyika Jijini hapa na kusema hali ya Halmashauri imekuwa mbaya kutokana na vitambulisho hivyo kugawiwa kwa wafanyabiashara wasi walengwa.
Alisema kuwa Jiji hilo lilikuwa na jumla ya vyanzo vya mapato 38 ambavyo vilikuwa vinatarajiwa kuliingiza Halimashauri hiyo bajeti ya Bil 15 lakini ugawaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wasio stahiki imesababisha kasoro hiyo.
Alidai chanzo cha kupelekea hali hiyo kimesababishwa na Watendaji wa kata na Mitaa kwa kushindwa kusimamia kwa ukaribu ugawaji wa vitambulishi hivyo kwa watu wanaostahili na badala yake wamewagawiwa hata wafanyabiashara wasihusika.
“Watendaji mmetuangusha mmegawa vitambulisho hata kwa wafanyabiashara wasiostahili na mmefanya hivyo ili kuvimaliza lakini ni athari kwetu hasa Halmashauri hatuna fedha na miradi mingi itakwama”Alisema Seleboss.
Aidha alisema watendaji  wamechangia kukwamisha ukusanyaji wa mapato ambapo yamefikia asilimia 65% huku ikiwa bado mwezi mmoja kumalizika kwa mwaka wa serikali uishe ilihali angalau ukusanyaji huo ulitakiwa ufikie 80%.
Alisema kuwa ukosefu huo wa mapato umesababisha Halimashauri hiyo kushindwa kutekeleza shughuli za kijamii kama usafi wa masoko pamoja na marekebisho ya taa za barabarani.
“Watendaji wameshindwa kutafsiri nia ya Rais kwani vitambulisho vimetolewa hadi kwa wavuvi pamoja na wafanyabiashara wakubwa wenye maduka sasa wote wamegeuka na kuwa wajasiriamali”alisema Mustafa.
Hata hivyo akiongelea upande wa leseni za biashara Meya Mustafa alisema kuwa wamepoteza mapato ya kiasi cha sh Mil 700 zilizokuwa zikusanywe kutokana na maombi ya leseni hizo lakini sasa wafanyabiashara wengi wamerudisha leseni hizo na kukata vitambulisho vya wajasiriamali.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Ramadhani Possi alisema kuwa ufinyu wa bajeti umesababisha miradi mingi ambayo walikuwa wamepanga kuitekeleza kushindwa kutekelezwa kwa wakati .
“Kwa sasa tunajipanga kuboresha miundombinu ya shule zetu kwa kujenga madarasa mapya ukarabati ya vyoo pamoja na madawati ambapo tunafanya kila pale tunapopata fedha japo kidogo”alisema Possi.
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Tanga Selemani Zumo aliwataka watendaji wa Jiji kuhakikisha wanafanyakazi kwa uwadilifu na kujituma pamoja na kujua mipaka ya kazi zao.
Alisema kuwa haiwezekani watendaji hao wakawa ni sehemu ya migogoro baina yao na viongozi wa kisiasa ambao wao wapo kwa ajili ya kuhakikisha wanasimami maslahi ya wananchi ambao ni wapiga kura wao.
Awali akichangia mada katika baraza hilo Diwani wa kata ya Mabawa Mwasabu Ngare alisema baadhi ya taa za barabarani haziwaki na hali hiyo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la vibaka na wananchi kupoteza mali zao.
Mwisho.
Share To:

Post A Comment: