Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Afrika ya Kusini, amekitangaza chama tawala nchini humo cha African National Congress (ANC) kuwa mshindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe nane mwezi huu.

Chama hicho kimepata ushindi wa asilimia 57.5 ikiwa ni mara ya sita mfululizo tangu kukomeshwa kwa utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo. Katika uchaguzi huo chama cha Democratic Alliance (DA) kilipata asilimia 20.8 huku chama cha Economic Freedom Fighters (EEF) kikipata asilimia 10.8 ya kura zilizopigwa.

Kwa mujibu wa viongozi wa ujumbe wa waangalizi katika uchaguzi huo, Rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete na Gudluck Jonathan wa Nigeria, uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: