Sunday, 5 May 2019

Haji Manara apangua shutuma za klabu ya Simba


Ofisa habari wa Simba Haji Manara, amepangua shutuma za klabu hiyo kutumia fedha na kupendelewa ili ipate matokeo uwanjani.

Manara ameyasema hayo katika kikao na waandishi katika ukumbi uliopo ndani ya Hoteli ya Pick jijini Mbeya.

Akizungumza juu ya tuhuma za Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera na Kocha wa Mbeya City Ramadhani Nsanzurwimo, amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwa makini na hizi tuhuma zinazotolewa na baadhi ya makocha wa ligi kuu.

“Sina maana ya kuwataka TFF kuwafungia hao makocha wanaotoa tuhuma ila wajaribu kutoa onyo ili haya mambo yasijirudie kwenye ligi yetu”amesema Haji Manara .

No comments:

Post a comment