Saturday, 11 May 2019

EALA WAKUTANA NA WAWAKILISHI WA WAKULIMA WADOGO EAC

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Martin Ngoga akizungumza na Wawakilishi wa wakulima wadogowadogo waliokutana leo Jijiji Arusha 
 Meneja Kampeni kutoka shirika la Oxfam Tanzania Jovitha Mlay akizungumza juhudi  mbalimbali zinazofanywa ili kuwakwamua wakulima wadogo haswa wakina mama ambao ni wengi na wapo zaidi ya 60%duniani kote wanaojishughulisha na Kilimo.

Elizabeth Ng'imo Katibu wa wakulima wadogo wanawake Afrika na mkulima kutoka Mkoa wa Kati Kenya
 Baadhi ya wawakilishi wa wakulima wadogowadogo kutoka katika Nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika ukumbi wa Bunge hilo leo walipokutana Jijini Arusha

Wawakilishi Wakulima wadogowadogo wa Jumuiya ya Afrika ya mashariki wamekutana na wabunge wa Jumuiya hiyo lengo likiwa ni kujaribu kushwishi nchi wanachama kuongeza bajeti katika sekta ya kilimo

Martin Ngoga Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika ya mashariki ambapo amesema  azimio la Malabo lililosainiwa mwaka 2014 Guinea ya Ikweta kati ya nchi 47 linazitaka nchi za Afrika katika bajeti zake zitenge walau 10%zielekezwe kwenye kilimo

Ngoga amesema kilimo ndiyo  uti wa mgongo wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na ndicho kinachotegemewa na wananchi walio wengi, hivyo  wanajadiliana na wadau wengine kuona ni jinsi gani wanaweza kwenda haraka zaidi  katika kutekeleza azimio hilo.

''Bado  Bunge la Afrika ya Mashariki tunaamini kwamba azimio hilo bado ni muhimu  japo kwa bahati mbaya Bunge halijafanya vizuri katika bajeti zao''alisema Ngoga.

Jovitha Mlay ni Kampeni Meneja kutoka shirika la Oxfam Tanzania amesema wanaungana na wadau wengine kwaajili ya kudai ongezeko la bajeti katika kilimo,pamoja na kuwataka nchi wanachama kutekeleza makubaliano ambayo wamesaini kwenye maazimio ya Malabo. 

Amesema ripoti iliyotoka inaonyesha nchi kadhaa katika Jumuiya ya Afrika ya mashariki hazijafikia kutenga hiyo 10% jambo ambalo lilitakiwa nchi wanachama ziwe tayari zimetenga na kusimamia ugawaji na matumizi ya fedha hizo katika sekta ya kilimo. 

Amesema Oxfam lengo lake kubwa ni kuitisha nchi washirika kuhakikisha kwamba wanawekeza kwa wakulima wadogo kwani ndiyo wengi wanalisha,kuzalisha chakula kinacholisha jamii ya nchi wanachama.

Amesema pia Oxfam inaangalia ushiriki wa wanawake katika utekelezaji na bajeti zinazotengwa kwani wapo zaidi ya 60%ya wakulima duniani kote,pia izingatie maswala ya utafiti,kutokana na mabadiliko ya tabia nchi,mbegu ,madawa na viwatilifu,pembejeo,miundombinu ya maji  ambayo ni muhimu .

 Elizabeth Ng'imo Katibu wa wakulima wadogo wanawake Afrika na mkulima kutoka Mkoa wa Kati Kenya amesema kuwa  changamoto kubwa katika sekta ya kilimo ni fedha hivyo wanaomba nchi wanachama kujitahidi kutenga hiyo bajeti kwaajili ya kuwasaidia wakulima wadogowadogo 

Spika wa bunge la Afrika mashariki  Martin Ngoga amesema kuwa agenda hiyo itakuwa ni miongoni mwa ajenda ambazo zitajadiliwa katika mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika mashariki unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na wadau wa kilimo yakiwepo mashirika yanayojihusisha na kilimo kama vile OXFAM, Action Aid na shirika la Trust Afrika

No comments:

Post a Comment