Thursday, 30 May 2019

DC Mjema azindua wiki ya Mazingira kwa kutoa elimuNA HERI SHAABAN
MKUU wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amezindua wiki ya Mazingira Wilaya ya Ilala  Dar es Salaam leo kwa kutoa elimu juu ya uhamasishaji kuhusiana na utunzaji wa Mazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam,katika utoaji wa elimu hiyo sambamba na utunzaji wa Mazingira ,utumiaji wa mifuko mbadala,upandaji miti.

"Katika Wilaya yangu ya Ilala tunazindua siku hii kwa kutoa elimu pamoja na upandaji miti na kampeni ya usafi katika maeneo mbalimbali ambapo kwenye wilaya yangu shughuli hizi shughuli zinafanyika wiki nzima Mei 29 hadi juni 42019"alisema Mjema.

Mjema alisema madhimisho hayo yanafanyika kila mwaka June 5 kimataifa siku ya Mazingira Duniani inafanyika China Kauli Mbiu mwaka huu "Pingana na uchafuzi wa hewa" .

Alisema inakadiliwa  uharibifu wa tabaka la hewa usababisha upungufu wa mazao nafaka kwa asilimia 26 ifikapo mwaka 2030.

Aidha alisema matumizi ya mifuko ya plastiki ni makubwa hata hivyo matumizi hayo yamekuwa na madhara mbalimbali kama vifo vya samaki ,mifugo,Wanyama pori,ndege,  madhara katika afya ya binadamu,kuziba kwa miundombinu,kusababisha mafuriko.

Akielezea madhara mengine  ya mifuko ya plastiki uchukua miaka 500 hadi 1000 kuoza katika arddhi,na kusababisha mfumo wa ikolojia kutokaa vizuri na kuathiri kilimo hivyo upelekea kupunguza uzalishaji mazao.

Alisema kutokana na madhara hayo Tanzania inaungana na nchi 60 Duniani kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki baadhi ya nchi hizo za Ukanda wa Afrika Mashariki ,Kenya,Rwanda.

Wakati huohuo alisema halmashauri ya Ilala  Mei 5 ilianza kutekeleza agizo la Waziri Mkuu kutekeleza Katazo la mifuko ya Plastiki kama agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa.

Katika utoaji wa elimu hiyo juu ya kupiga marufuku mifuko ya plastiki halmashauri imefanya juhudi mbalimbali ikiwemo kuunda timu ya wataalam kufatilia katazo la mifuko ya Plastiki   ikiwemo kuweka mikakati mbalimbali pamoja na kuanisha jinsi ya taratibu za upokeaji wa mifuko hiyo ngazi ya Kata vituo vimetengwa 36 na vituo vya makampuni vinane.
Mwisho

No comments:

Post a Comment