Tuesday, 28 May 2019

DC Kongwa Ampongeza Rais Magufuli


Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi amempongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wake wa busara wa kuamua kuwatambua wajasiriamali wadogo kwa kuwatengenezea vitambulisho maalumu.

Ndejembi amesema vitambulisho hivyo vimekuwa na msaada mkubwa sana kwa wajasiriamali wa wilaya yake kwani hivi sasa hawalipi tozo yoyote na wanafanya biashara bila kubughudhiwa.

Akitoa taarifa ya namna walivyouza vitambulisho hivyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge, DC Ndejembi amesema wameendesha zoezi hilo vizuri na kuahidi kuendelea kuwafikia wajasiriamali wote katika maeneo yao ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anapata kitambulisho hicho.

Kwa upande wake RC Mahenge ameipongeza wilaya hiyo kwa kuendesha zoezi hilo vizuri ukilinganisha na wilaya nyingine za Mkoa huo.

No comments:

Post a Comment