Deonald Dea Afisa mtendaji  mkuu wa chama cha Wanasheria wa Afrika (PALU)

Na.Vero Ignatus Arusha.

CHAMA cha Wanasheria wa Afrika  (PALU) kwa kuahirikiana na Taasisi zingine ikiwemo inayosimamia matumizi ya kidijitali  Duniani Article 19,  wamekutana Jijini Arusha kwa ajili ya kujadili na kuweka mikakati ya kusimamia haki za watumiaji wa mitandao ya teknolojia ya kidijitali, ili kuwezesha wananchi wa nchi hizo kupata huduma.

Deonald Dea ni Afisa mtendaji  mkuu wa chama PALU ambapo amesema kuwa, binadamu wana haki ya kupata huduma ya mawasiliano  ya kidijitali  ili waweze kuendesha shughuli za kibinadamu vizuri.

Deya alishauri  badala ya serikali kukimbilia kufunga  mitandao hiyo, wangeiachia  Bunge lipitishe sheria nzuri za kusimamia suala hilo na huku Mahakama zikihakikisha zinapewa nafasi za kuhakikisha sheria hizo zinasimamiwa na anayekiuka anapata stahiki yake

Dea amesema kuwa Mawasiliano ni muhimu kwa wakati kama huu sababu mitandao inatumika katika kufanya biashara ,kutoa elimu na hata maswala ya Afya pamoja na mengine mengi.

"Sisi  kama binadamu tuna uhuru wa kuzungumza na uhuru wa kupata taarifa sahihi na kwa mfumo wa sasa wa  kutumia mawasiliano ya kidijitali  kama Intenet ndio njia kubwa za kusambaza habari na hapo kuna sheria zinazotakiwa kuwepo  ili kulinda uhuru huu kwa binadamu,”alisema"

Amesema wamekutana wanasheria, wanaharakati, toka nchi za EAC na Maofisa wa haki za binadamu wa jumuiya ya Afrika ya mashariki na  Tume ya umoja wa Afrika ya kupambana na Rushwa ,na Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu na kijamii .

"Kwani kweli hata serikali inatumia mitandao hii kufanikisha kukamata wahalifu wa makosa mbalimbali , hivyo vema kila upande ukaheshimu haki ya wengine na sio kukimbilia kuzuia  wngine wasipate haki  ya mawasiliano,”alisema  

Amesema kuwa pamoja na haki hizo bado zipo baadhi ya serikali ya nchi hizo zinakiuka haki za binadamu za uhuru wa kuhakikisha wanapata mawasiliano kwa kufunga mitandaobya kijamii wakihofia kukashifiwa jambo balo siyo sahihi

Ephraim Kenyanito kutoka Afisa mipango wa kidigitali kutka Article 19 ya nchini Kenya kuwa ni vyema kukawepo na sheria zitakazowasaidia wananchi kutumia vizuri teknoloji kuweza kupata mawasiliano ya haraka na kufanya biashara.
“Hadi sasa  hatuwezi   kuzifikia nchi zilizoendelea katika matumizi ya kidijitali kwenye masuala mbalimbali , hivyo vema na nchi zetu za EAC  tukafanya   jitihada kuweka mipango madhubuti ya kusimamia hili na kueneza huduma hizo za mtandao kwa  wananchi wote wa nchi za EAC, na hasa vijijini,”alisema
Mwisho
Amesema hivi sasa katika nchi nyingi wanawake wananwake hawajaunganishwa kutumia teknolojiankama wanaume hivyo watafiti watumie sheria jinsi ya kufanya ili watu watumie mitandao.
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: