Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa, Stephen Mhapa  akiwa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Robert Masunya wakati wa baraza la madiwani wakijadili kuhusu athari za wanyama Tembo na Boko
 Madiwani na wataalam wa halmashauri ya wilaya ya Iringa wakiwa kwenye baraza kujadili athari zitikanazo na wanyama Tembo na Boko

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

JUMLA ya wananchi saba wameuwawa na mnyama aina ya Boko ndani ya mwezi mmoja katika bwawa la Mtera lililopo katika tarafa ya Ismani halmashauri ya wilaya ya Iringa huku pia mnyama aina ya Tembo akiendelea kuharibu mazao ya wakulima wa halmashauri hiyo.

Akizungumza katika baraza la madiwani ,diwani wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi kutoka katika tarafa ya Ismani Yusta Kinyanga alisema kuwa mnyama aina ya Boko wamezaliana kwa kasi kubwa na kuwa wengi katika bwawa la Mtera na kusababisha vifo vya wananchi kutoka na wingi wao.

“Saizi Boko hao wapo wengi mno katika bwawa hili la Mtera na kusababisha vifo vya wananchi ambavyo havina tija yoyote na kupunguza nguvu kazi za taifa kwa kuuwawa na book hao” alisema Kinyanga

Kinyanga alisema kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli aliagiza mamlaka zinazohusika kuhakikisaha wanavuna Boko hao ili kupunguza vifo vya wavuvi wanaofanya shughuli zake katika bwawa hilo.

“Alipokuwaja Rais hapa nilimweleza juu ya swala hili la Boko na aliziagiza mamlaka husika kushughulikia swala hilo lakini toka alipoondoka Rais hadi sasa wananchi saba wameuuwawa kwa maana hiyo mamlaka husika zimepuuza tamko la Rais na kusababisha vifo hivyo vya wananchi” alisema Kinyanga

Kinyanga ameiomba mamlaka zinazohusika kuhakikisha wanawavuna Boko hao ili kupunguza vifo vya wananchi vinavyosababisha kuacha wanawake wengi kuwa wajane kutokana na wanaume zao kuuwa na viboko hao.

“Wanaofanya kazi ya uvuvi ni wanaume ambao kwa asilimia kubwa wameshaoa na wanafamilia  hivyo kuuwawa kwa wanaume hao kuwanawacha wanawake kuishi bila wanaume zao hivyo kumpelekea mwanamke huyo kuwa mjane” alisema Kinyanga

Naye diwani wa kata ya Ilolo mpya,Fundi Mihayo amesema kuwa wanyama wa aina ya tembo wamefanya uharibifu wa mazao wa wananchi wa kata hiyo kutokana na kuwepo kwa kundi kubwa na Tembo ambao wanafanya uharibifu wa mazao ya wananchi.

“Mwaka huu kundi kubwa hili la tembo hatujui limetoka wapi na limekuja kuleta athari za mazao kwa  wananchi wetu na mamlaka husika hakuna jitihada yoyote ile ambayo wanaifanya kuhakikisha wanakabiliana na tembo hao” alisema Mihayo

Mihayo alisema athari nyingine ambayo imejitokezani kushindwa kwa wanafunzi kwenda shuleni kwa kuhofia kudhuliwa na Tembo ambao wamekuwa wakitembea katika maeneo hao ambao wanafunzi hao ndio njia kuu ya kuelekea shuleni.

“Saizi wanafunzi wanaogopa hata kwenda shule maana njia zote ambazo wanafunzi huwa wanapita kwenda shule ndio njia ambazo kwa sasa tembo ndio maeneo ambayo wanashinda kutafuta chakula na wameweka makazi yao” alisema Mihayo

Kwa ujumla mwaka huu hadi hivi sasa Tembo hao wameshafanya uharibifu wa mazao katika kata ya Ilolo Mpya,Nzihi na kata ya Kiwele na kuwaacha wananchi wasijue cha kufanya kutokana na kuwepo kwa Tembo hao.

Kwa upande afisa maliasilia wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Evidence Machenje alisema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha wanawavuna Boko kutokana na taratibu na sheria za wanyama pori hivyo tayarai wamewasilisha taarifa hizo kwa wizara na wanasubiri majibu kutoka wizarani.

“Ni kweli tunataarifa za athari zinazotokana na Boko hao hivyo sisi kama halmashauri hatuna mamlaka ya kuwavuna wanyama hao hivyo ni lazima tuwasiliane na mamlaka husika ili waje wafanyae utalamu wao ndipo lije swala la uvunaji wa Boko hao” alisema Machenje

Aidha Machenje amekili kuwa Tembo na Boko wamefanya uharibifu mkubwa na kuleta madhara makubwa kwa wananchi lakini kila kitu kinaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi hivyo wananchi wanatakiwa kuwa na subira muda mfupi ujao kila kitu kitakuwa tayari kimefanyiwa kazi.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa, Stephen Mhapa alimwagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa matatizo hayo ya wanyama hao yanatafutiwa ufumbuzi mapema iwezekanavyo ili kuokoa maisha ya wananchi

Hata mimi ni mwadhirika kwenye kata yangu kwa Tembo kuaribu mazao ya wananchi hiki kitendo kinakera hivyo wataalam naombeni fanye haraka kuwasiliana na mamlaka husika kutatua tatizo hilo
Share To:

Post A Comment: