Na Rahel Nyabali-Tabora.

Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri ametoa onyo kwa mtu yeyote atakayeshiriki katika uharibifu wa mazingira hasa ukataji wa miti.

Ameyasema hayo wakati akishiriki zoezi la upandaji wa miti na wanafunzi wa chuo cha Tekinolojia cha Dar es Salaam D.I.T katika  Kata ya Kanyeye manispaa ya Tabora ikiwa ni juhudi za kuboresha mazingira, uhifadhi vyanzo vya maji na kuifanya Tabora kuwa ya kijani.


“Mtu yeyote atakayekamatwa atasukumwa ndani,tunachofanya hapa ni kuotesha miti kila Halimashauri inavitalu vyake kuanzia mkuu wa mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mtendaji wa kata mtendaji wa kijiji hadi mtendaji wa mtaa, tunataka tuhakikishe miti hii inapandwa katika taasisi zote” amesema.

Kwa upande wake kiongozi wa wanafunzi  kutoka chuo cha D.I.T, Machage Emmanueli amesema lengo la kushiriki zoezi la upandaji wa mti ni kuimarisha uoto wa asili  nakuzidi kuwa kijani.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: